Total Yafanya Kweli, Yazindua Kituo cha Kisasa cha Mafuta, Total Kilimanjaro, Kijijini cha Samanga, Marangu, Moshi, Kilimanjaro.

  Masama Blog      
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjara,  Anna Mghwira, (katikati) akizindua kituo kipya cha mafuta na huduma cha Total Kilimanjaro, katika kijiji cha Samanga, kilichopo Marangu mkoani Kilimanjaro ambacho kinamilikiwa na mfanyabiashara mzawa kwa asilimia 100%, ila kimejengwa kwa ushirikiano na kampuni ya mafuta ya Total Tanzania katika utaratibu unaitwa DODO. Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Total Tanzania Jean Franchois Schoepp, Meneja Mawasiliano wa Total, Marsha Msuya Kileo Meneja wa Mtandao wa vituo vya mafuta vya Total, Marriame Sow. Kushoto kwake ni mmiliki wa kituo hicho , Eliawony Towo, Mke wake, na Mwenyekiti wa Bodi ya kituo hicho Bw, Mawalla.


Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjara, Anna Mghwira, akijaza mafuta gari kuashiria uzinduzi wa kituo kipya cha mafuta na huduma cha Total Kilimanjaro, katika kijiji cha Samanga, kilichopo Marangu mkoani Kilimanjaro ambacho kinamilikiwa na mfanyabiashara mzawa kwa asilimia 100%, ila kimejengwa kwa ushirikiano na kampuni ya mafuta ya Total Tanzania katika utaratibu unaitwa DODO. Nyuma yake ni Mkurugenzi Mtendaji wa Total Tanzania Jean Franchois Schoepp, Meneja Mawasiliano wa Total, Marsha Msuya Kileo Meneja wa Mtandao wa vituo vya mafuta vya Total, Marriame Sow na mke wa mmiliki wa kituo hicho , Eliawony Towo.


Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjara,  Anna Mghwira akijaza mafuta boda boda kuashiria uzinduzi wa kituo kipya cha mafuta na huduma cha Total Kilimanjaro, katika kijiji cha Samanga, kilichopo Marangu mkoani Kilimanjaro ambacho kinamilikiwa na mfanyabiashara mzawa kwa asilimia 100%, ila kimejengwa kwa ushirikiano na kampuni ya mafuta ya Total Tanzania katika utaratibu unaitwa DODO. Nyuma yake ni Mkurugenzi Mtendaji wa Total Tanzania Jean Franchois Schoepp, na Meneja wa Mtandao wa vituo vya mafuta vya Total, Marriame Sow na mke wa mmiliki wa kituo hicho , Eliawony Towo.

Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro,  Anna Mghwira, Kushoto na Mkurugenzi Mtendaji wa Total Tanzania Jean Franchois Schoepp wakipanda mti wa kumbukumbu kuashiria uzinduzi wa kituo kipya cha mafuta na huduma cha Total Kilimanjaro, katika kijiji cha Samanga, kilichopo Marangu mkoani Kilimanjaro ambacho kinamilikiwa na mfanyabiashara mzawa kwa asilimia 100%, ila kimejengwa kwa ushirikiano na kampuni ya mafuta ya Total Tanzania katika utaratibu unaitwa DODO. Nyuma wanaoshuhudia ni Meneja Mawasiliano wa Total, Marsha Msuya Kileo Meneja wa Mtandao wa vituo vya mafuta vya Total, Marriame Sow. Kushoto na mke wa mmiliki wa kituo hicho, Eliawony Towo.Watanzania, wamehimizwa kuchangamkia fursa za biashara kwa ushirikiano na makampuni makubwa yenye mafanikio, kama kampuni ya Total Tanzania, ili wafanyabiashara wa kitanzania waweze kukuzwa kwa viwango vya kimataifa.
Wito  huo umetolewa leo, na Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjara, Anna Mghwira, wakati wa uzinduzi wa kituo kipya cha mafuta na huduma cha Total Kilimanjaro, katika kijiji cha Samanga, Marangu mkoani Kilimanjaro, ambacho kinamilikiwa na mfanyabiashara mzawa kwa asilimia 100, ila kimejengwa kwa ushirikiano na kampuni ya mafuta ya Total Tanzania. ambacho kitauza mafuta, vilainishi  na kutoa huduma ikiwemo kufanya service za magari
 Bibi Anna Mghwira amesema, “Tunapopata wawekezaji wenye kutoa fursa kwa wafanyabiashara wazawa ya kushirikiana nao katika kuleta maendeleo kama ambavyo Total wanafanya, ni jambo zuri na la kuigwa na makampuni mengine” .
Pia Mkuu wa Mkoa, alimpongeza mmiliki wa kituo hicho, “Nakupongeza sana bwana Eliawony Towo, na ni matumaini yangu wafanyabiashara wengine wa Kilimanjaro mtachangamkia fursa na tutaona vituo vingine kama hivi kwenye maeneo ya ndani ambako huduma kama hizi hazijafika ili kuchochea maendeleo na pia kusaidia kuongeza ajira kwa wanajamii wa eneo husika”.
Akiongea wakati wa uzinduzi wa kituo hiko, Mkurugenzi Mtendaji wa Total Tanzania Jean Franchois Schoepp amesema "Total tumedhamiria kuwafikia Watanzania wengi zaidi kwa kuwapatia na fursa ya kupata huduma bora kutoka katika vituo vyetu vyenye mafuta bora ya Total Excellium na bidhaa zenye ubora. Tunawaalika wafanyanyabashara ambao wanamiliki vituo vya mafuta na wapo tayari kushirikiana nasi kibiashara kuchangamkia fursa hii  kupitia mpango wetu wa DODO.
tunatoa wito kwa wafanyabiashara wengine, kujitokeza ili kuwapa fursa zaidi Watanzania kufaidika na bidhaa bora za Total ili zisambae zaidi na kupanua masoko yetu zaidi” alisema Schoepp.
Kwa upande wake mmiliki wa kituo hicho , Eliawony Towo, aliishukuru kampuni ya Total Tanzania kwa kumpatia fursa hiyo na kuahidi kutoa huduma bora za kiwango cha Total na sio tuu kuuza mafuta, vilainishi  na kutoa huduma ikiwemo kufanya service za magari,  bali pia atafungua duka la Total na kufungua mgahawa wa Bonjou ambao utauza kahawa ya Kilimajaro kwa mfumo wa cappuchino na expresso inayopendwa na watalii.
Meneja wa Mtandao wa vituo vya mafuta vya Total, Marriame Sow amesema uzinduzi wa kituo hiki ni katika utekelezaji wa mpango wa biashara wa kampuni ya mafuta ya Total kupanua wigo wa biashara yake nchini katika kusambaza huduma za Total zienee nchi nzima. Kituo hiki kipya cha Total Kilimanjaro kiko kando ya Barabara ya Himo-Marangu na kinalenga kuwahudumia watu wa Marangu na maeneo ya jirani kupata huduma bora kutoka vituo vya Total yakiwemo mafuta bora  yenye kiambata cha Total Execellium na bidhaa bora za vilanishi vya Total.
Meneja Mawasiliano wa Total, Marsha Msuya Kileo, amesema Kituo cha Total Marangu, ni moja ya vituo vipya vya Total vinavyoendeshwa kwa ubia kati ya kampuni na mfanyabiashara  mzawa (DODO)  ambapo kituo hiki ni cha kwanza cha mfumo huu katika mkoa wa Kilimanjaro.
Uzinduzi huo umehudhuriwa na viongozi na wananchi wa kijiji cha na kimeanza kwa kutoa zawadi ya mafuta, kwa kila lita ya mafuta mteja akinua unaongezewa lita moja ya bure.
Total Tanzania ndio kampuni inayoongoza kwa uuzaji wa mafuta nchini Tanzania kufuatia kumiliki vituo zaidi ya 100 vya mafuta vinayotoa huduma za usambazaji na uuzaji wa mafuta ya petroli, dizeli vilainishi na bidhaa za mafuta. End.

from MICHUZI BLOG https://ift.tt/2v98MoQ
via
logoblog

Thanks for reading Total Yafanya Kweli, Yazindua Kituo cha Kisasa cha Mafuta, Total Kilimanjaro, Kijijini cha Samanga, Marangu, Moshi, Kilimanjaro.

Previous
« Prev Post