TECNO ilivyosherehekea Siku ya Wapendanao na wateja wake

  Masama Blog      
Katika kusherehekea siku ya Wapendanao, kampuni ya simu za mkononi TECNO ilisherehekea siku hii maarufu ya Valentine na wateja wake wa   simu za TECNO SPARK4, CAMON 12 na CAMON12 AIR, pamoja na fans wake kutoka kurasa zake za mitandaoni kwa kuwapeleka sehemu mbalimbali maalum kwaajili ya kuvinjari mwishoni mwa wiki.
Tukio hili maalum liliandaliwa kwaajili ya kuwakutanisha watu wawili wa jinsia tofauti pasipo kufahamiana yaani blind date. Kabla ya kupelekwa katika hoteli ambayo iliandaliwa kwaajili ya kupata dinner, yule wa jinsia ya kike alipelekwa kufanyiwa makeup katika saluni maarufu na yenye hadhi na mwanaume alipelekwa katika duka la nguo maarufu.
Akizungumza wakati wa chakula cha jioni dinner mshindi wa kike Bi. Queen Alfred aliishukuru kampuni ya TECNO kwa kuandaa tukio hili huku akiwasisitiza wadau wote wa TECNO kufuatilia kurasa za TECNO mtandanoni ili kupata fusa kama alivyopata yeye na nyingine nyingi zaidi.
“Nawashukuru sana TECNO nimefurahi sana kwa kunipa nafasi ya kunifanyia make up, kunipendezesha na kunileta hohelini kwaajili ya dinner, mwanzoni walipotangaza kwenye ukurasa wa Instagram sikuwa naamini lakini kumbe ni kweli” Alisema Queen
Naye mshindi wa kiume Bw. Kalebo Ibrahim aliishukuru TECNO kwa nafasi aliyoipata ya kuvalishwa na TECNO katika duka kubwa la nguo.
“Kwanza nafurahia sana kutoka out na TECNO na kunileta kwenye duka la pamba kali na kikubwa kunikutanisha na mtu nisiyemfahamu na sasa tumefahamiana. Ninachowashauri watu wazidi kutembelea kurasa za TECNO mitandaoni ili kupata habari za fursa” alisema Kalebo.
Katika Valentine ya 2019, TECNO iliwapeleka wateja wake kutembelea maeneo mbalimbali ya kitalii visiwani Zanzibar kwaajili ya mapumziko bila wao kuchangia gharama yoyote. Mpaka sasa TECNO inaendelea na kampeni ya kuwapandisha wateja wake kwenye helikopta mwezi Machi.
Washindi wa TECNO Valentine Blind Date wakifurahia kwa pamoja baada ya kukutanishwa. 
 Kalebo Ibrahim na Queen Alfred washindi wa TECNO Blind date wakipeana maua ishara ya kuanza kufahamiana baada ya kukutanishwa bila wao kufahamiana.
 Mwonekano wa Bi. Queen baada ya kufanyiwa make up
Mwonekano wa Bw. Kalebo baada ya kuvaa nguo kwenye moja ya maduka maarufu ya nguo.


from MICHUZI BLOG https://ift.tt/3bX2vgS
via
logoblog

Thanks for reading TECNO ilivyosherehekea Siku ya Wapendanao na wateja wake

Previous
« Prev Post