TANZANIA MIONGONI MWA NCHI ZINAZOKUSUDIA KUREJESHA UOTO WA ASILI TAKRIBANI HEKTA MILLION 5.2

  Masama Blog      


Afisa mazingira mkuu kutoka ofisi ya makamu wa Rais Fainahappy Makambo akiwasisitiza wadau kuhakikisha wanatekeleza mikakati watakayoijadili ili kurejesha uoto wa asili na kuunga mkono malengo ya dunia ya kurejesha uoto wa asili hekta 350 ifikapo mwaka 2030 kushoto kwake kwenye picha ni wakala wa huduma za misitu nchini Dkt, Hamza Katety .na kulia kwake ni Dk Lawrence Mbwambo.
Mratibu wa progamu ya mazingira na mshauri wa sera shirika la maendeleo na uhifadhi wa mazingira WWF Dkt.Lawrence Mbwambo akieleza kwa wadau waliokutana mkoani Morogoro kujadili namna ya kurejesha uoto wa asili amesema uaribifu wa ardhi unakadiliwa kuwa takribani asilimia 61.

Wadau wa mazingira wakisikiliza kwa makini afisa mazingira mkuu
Fainahappy Kimambo (hayupo pichani )mikakati ya serikali katika kuhakikisha wanarejesha uoto wa asili kwa hekta milioni 5.2 ifakapo mwaka 2030 .

wadau wa mazingira waliokutana mkoani Morogoro kujadili namna ya kurejesha uoto wa asili wakiwa katika picha ya pamoja na mgeni rasmi ambaye ni Afisa mazingira mkuu ofisi ya makamu wa Rais Fainahappy Kimambo.

 


Tanzania imekubalina na mpango wa dunia wa kurejesha uoto wa asili hekta millioni 5.2 kati ya millioni 350 ambazo nchi zote duniani zimejipanga kurudisha uoto huo ulipotea kwa sababu mbalimbali ikwemo shughuli za kibinadamu.

Wadau wa mazingira wamekutana mkoani morogoro kujadli jinsi ya utekelezaji wa kuhifadhi na kurudisha uoto wa asili ambapo Afisa wa mazingira, mkuu wa ofisi ya Makamu wa Rais,Fainahappy Kimambo amesema nchi za Afrika zimelenga kurejesha uoto wa asili kiasi cha hekta milioni 100 ifikapo mwaka 2030 .
 
Ambapo kidunia hekta milioni 350 na Tanzania imepewa lengo la kurejesha uoto wa asili hekta million 5.2 huku wakala wa huduma za misitu nchini Dk Hamza Katety amesema kiwango cha uharibifu wa misitu ni kikubwa na wanakusudia kupanda miti kwa kushirikiana na taasisi nyingine


from MICHUZI BLOG https://ift.tt/2Snf0dT
via
logoblog

Thanks for reading TANZANIA MIONGONI MWA NCHI ZINAZOKUSUDIA KUREJESHA UOTO WA ASILI TAKRIBANI HEKTA MILLION 5.2

Previous
« Prev Post