Taasisi ya Jangwani to Forest Movement yapanda miti 50 katika Shule mbili

  Masama Blog      

Na Chalila Kibuda,Michuzi Globu.

Wanafunzi wakipata elimu ya utuzaji wa Mazingira ni hazina ya taifa katika kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi.

Hayo aliyasema Mwasisi wa Jangwani to Forest Movement Verdiana Nsongo wakati wa upandaji wa miti katika Shule za Msingi za Msisiri na Kinondoni zilizopo Manispaa ya Kinondoni jijini Dar es Salaam.

Amesema kuwa misingi bora ya utunzaji mazingira ni kutoa elimu kwa  wanafunzi kuanzia katika maeneo yao shule ambapo wanaoweza kwenda kutoa elimu katika jamii wanazozizunguka

Nsongo amesema kuwa upandaji wa miti katika Shule mbili hizo ni mwendelezo wa Taasisi ya Jangwani to Forest Movement  kufikisha elimu ya utunzaji mazingira.

Amesema mafuriko yanayotokea ni kutokana na jamii imeacha kutunza Mazingira kwa kufanya Shughuli za kibidamu katika mkondo ya maji ikiwemo na ukataji miti hovyo.

Aidha amesema kuwa athari za kutotunza mazingira ni nyingi hivyo Vizazi na Vizazi lazima vipate elimu ya kutunza Mazingira.

Afisa Misitu wa Manispaa ya Kinondoni  Rogart Kimario amesema kuwa wanafunzi ni nguzo muhimu kuwekeza katika elimu ya mazingira.

Amesema kuwa wanafunzi wakianza kujengewa uwezo wa utunzaji mazingira kadri wanavyokuwa watakuwa wanaelewa elimu hiyo.

Nae Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Msisiri Emmanuel Kalula amesema kuwa Taasisi ya Jangwani to Forest Movement imefanya jambo lenye faida kwa Wanafunzi kupata elimu ya utunzaji mazingira.
Amesema kuwa kuna miti hiyo wataituza kwa Usimamizi wa pamoja na Wanafunzi ili waelewe na kuona faida wanazozipata kwa kuwapo kwa miti hiyo.
 Mwasisi wa Jangwani to Forest Movement Verdiana Nsongo akizungumza na Wanafunzi wa Shule za Msingi za Msisiri na Kinondoni wakati wa upandaji wa miti katika Shule hizo.

 Mwasisi wa Taasisi ya Jangwani to Forest Movement Verdiana Nsongo akipanda moja ya mti katika Shule ya Msingi Msisiri ikwa ni Kampeni ya utunzaji wa Mazingira wa Taasisi hiyo.
 Picha ya pamoja kati ya Walimu,Wanafunzi waliokaa na wadau wa Mazingira wa Taasisi ya Jangwani to Forest Movement.
 Mwanafunzi wa Darasa la Nne Shule ya Msingi Msisiri Taliq Bakari akipata mti katika Shule hiyo.
 Afisa Misitu wa Manispaa ya Kinondoni Rogart Kimario akipanda mti katika Shule ya Msingi Kinondoni ukiwa  ni Kampeni utunzaji wa Mazingira.
 Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Kinondoni Adeline Kessy akipanda mti katika Shule hiyo ikiwa ni Kampeni ya Taasisi ya Jangwani to Forest Movement utunzaji wa Mazingira.
 Afisa Misitu wa Manispaa ya Kinondoni Rogart Kimario akizungumza umhimu wa upandaji miti kwa Wanafunzi wa Shule za Msingi za Msisiri na Kinondoni.
 Picha ya pamoja kati ya  Walimu wa Shule za Msingi za Msisiri na Kinondoni pamoja na wadau wa Mazingira wa Taasisi ya Jangwani to Forest Movement.
Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Msisiri Emmanuel Kalula akipanda mti katika Shule hiyo ikiwa ni Kampeni ya Taasisi ya Jangwani to Forest Movement katika utunzaji wa Mazingira.
 


from MICHUZI BLOG https://ift.tt/37xD81x
via
logoblog

Thanks for reading Taasisi ya Jangwani to Forest Movement yapanda miti 50 katika Shule mbili

Previous
« Prev Post