STAR WA KIBAO CHA OOH MAMU APATA AJALI MBAYA

  Masama Blog      
     Na.Khadija seif, Michuzi Tv

MSANII wa singeli Mwarami Sadick maarufu Kama meja kunta alietamba na kibao cha ooh mamuu amepata  ajali alfajiri ya kuamkia leo maeneo ya segera mkoani Tanga.

Akizungumza na Michuzi Tv kupitia simu Meneja wa Meja Waso wiso amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo.

"Tumepata ajali maeneo ya segera Tanga na kwenye gari tulikua na cameraman,dj ,mimi pamoja na Meja mwenyewe tumegongana na gari ambapo ajali inatokea meja alikua amelala na yeye ndio ameumia sana,"

Hata hivyo waso wiso amesema ilikua ngumu kwao kupata msaada wa haraka kutokana na ilikua asubuhi sana na kumtaja madee pamoja na Naibu waziri wa maji Juma Aweso kuwa msaada kwao.

"Madee alikua ni miongoni mwa wasanii ambao walikua wanaelekea kwenye Tamasha la Muziki mnene hivyo ikawa rahisi kutuona barabarani akisaidiana na Naibu waziri wa maji Juma Aweso na kutupatia msaada wa haraka.

Hata hivyo Waso ameeleza kuwa Hali ya Meja sio nzuri hivyo wamelazimika kumkimbiza hospitali ya mkoa ili kupatiwa matibabu zaidi.


from MICHUZI BLOG https://ift.tt/2GOpJHm
via
logoblog

Thanks for reading STAR WA KIBAO CHA OOH MAMU APATA AJALI MBAYA

Previous
« Prev Post