SISI NI SAWA, TASI, ASAS WAPIMA KANSA YA NGOZI KWA WATOTO ZAIDI YA 286

  Masama Blog      

Na Avila Kakingo, Globu ya Jamii
WATU wengi wenye Ualbino hufariki dunia kwa kansa ya Ngozi  hivyo taasisi ya Sisi ni Sawa wakishirikiana naTaasisi ya watu wenye ualbino TAS na Kampuni ya Maziwa ya ASAS  imefanya uchunguzi  wa kansa ya Ngozi kwa watoto zaidi ya 286 katika hospitali ya Ocean Road jijini Dar es Salaam leo. 

Akizungumza na Mwandishi wa Michuzi Blog, Afisa Mtendaji Mkuu wa Tasisi  ya Sisi ni Sawa, Henry Mdimu amesema kuwa kansa ya ngozi inawaathiri zaidi watu wenye ualbino kutokana na mwanga wa jua kupenya kiurahisi zatika ngozi zao.

"Lengo kuu la kupima kansa ya ngozi kwa watu wenye Ualbino ni kuhakikisha tunapunguza vifo hasa vinavyosababishwa na kansa ya ngozi". Amesema Mdimu.

Hata Hivyo ametoa wito kwa watu wenye Ualbino kufika kila inapowezekana katika Hospitali ya Ocean Road kupima ngozi zao ili kama tatizo lipo liweze kutibiwa mapema na kuchukua tahadhali ya kutembea juani kwa muda mwingi.

Kwa Upande wake Mkuu wa Idara ya Afya katika Taasisi ya watu wenye ualbino (TAS), Mohamed Chanzi, amesema kuwa kuna kriniki wanazifanya kila siku ya Alhamis Katika Hospitali ya Ocean Road kwa watu wenye ualbino kwa watu wa Mkoa wa Dar es Salaam, hivyo kila mtu mwenye Ualbino anaweza kupata huduma hiyo.

"Leo tunapima afya ya Ngozi kwa watu wenye Ualbino ikiwa ni maadhimisho ya siku ya Saratani ambayo hufanyika kila mwaka Februali 4 ingawa leo tumefanya kwasababu tulichelewa kupata wahisani, na tumechelewa kufanya na wenzetu ndio maana tunafanya leo".

Tunapima Saratani ya ngozi kwa watoto ili tuweze kupambana na tatizo hilo mapema kwa maana mtu mwenye umri mkubwa inakuwa ngumu zaidi kutibia kwani inakuwa imeshafika kiwango kikubwa". Amesema Chanzi.

Chazi amesema kuwa mtu mwenye ualbino akiona tatizo lolote la ngozi awahi katika hospitali ya Ocean Road kwaajili ya kupata vipimo.

Hata  hivyo mwakilishi kutoka ASAS, Grolia Shao amesema wameona harakati za watu wenye Ualbino na kuwaunga mkono kwa kupima afya za ngozi zao ili waweze kugundua mapema kama wanamatatizo kwenye ngozi na waweze kutibiwa mapema.

Licha ya kupima afya ya zongo za watoto ASAS, TAS na Taasisi ya Sisi ni Sawa wameweza kuwapa mafuta kwaajili ya ngozi watoto wenye ualbino pamoja na Kofia za kujikinga na jua pale wanapotembea Juani.

Nae Mwanafunzi wa shule ya Msingi Jeshi la Wokovu, Ally Said Ally amewashukuru Taasisi ya Sisi ni Sawa, TAS na Asas kwa kuwapa vitu vya kijikinga na kansa ya ngozi pamoja na mafuta.

 Afisa Mtendaji Mkuu wa Tasisi  ya Sisi ni Sawa, Henry Mdimu  akizungumza na watoto wakati akiwapa maelekez ya jinsi ya kujikinga na maradhi ya ngozi watoto wenye Ualbino katika Hospitali ya Ocean Road jijini Dar es Salaam leo.
 Wanafunzi wakipima afya ya ngozi.


 Mwakilishi wa Asas, Grolia Shao akimvisha mtoto Kofia kwaajili ya kujikinga na jua.
Mtoto akijivinjari Maziwa ya Asas.


from MICHUZI BLOG https://ift.tt/3bibSr9
via
logoblog

Thanks for reading SISI NI SAWA, TASI, ASAS WAPIMA KANSA YA NGOZI KWA WATOTO ZAIDI YA 286

Previous
« Prev Post