Rwanda yasitisha mashtaka dhidi ya raia 17 wa Uganda

  Masama Blog      
Wizara ya Mambo ya Nje ya Rwanda imetangaza kuwa, nchi hiyo imesitisha mashtaka dhidi ya raia 17 wa Uganda waliokamatwa nchini humo.

Hatua hiyo inakuja siku moja baada ya kuachiliwa huru raia 13 wa Rwanda waliokuwa wanashikiliwa nchini Uganda.

Taarifa hiyo imesema kupitia ubalozi wake mjini Kampala, serikali ya Rwanda imekaribisha kuachiwa huru kwa raia wake 13 na kurejeshwa Rwanda watuhumiwa wawili wa ugaidi waliohusika na shambulizi la Kinigi lililotokea Oktoba mwaka 2019.

Mapema mwezi huu, Rwanda na Uganda zilikubaliana kubalishana wafungwa ikiwa ni mojawapo ya njia za kuimarisha tena uhusiano kati ya nchi mbili hizo ambao umekuwa ukilegalega.

Hatua hiyo ilifikiwa baada ya mkutano kati ya Marais Yoweri Museveni wa Uganda na Paul Kagame wa Rwanda uliofanyika katika mji mkuu wa Angola Luanda na kushuhudiwa pia na mwenyeji wao Joao Lourenco, na Felix Tshisekedi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.


from MICHUZI BLOG https://ift.tt/2SJ2WUn
via
logoblog

Thanks for reading Rwanda yasitisha mashtaka dhidi ya raia 17 wa Uganda

Previous
« Prev Post