Rais mstaafu wa Kenya Daniel Arap Moi afariki dunia

  Masama Blog      
Rais Mstaafu wa Kenya Daniel Arap Moi afariki dunia akiwa na miaka 95, rais Uhuru Kenyatta athibitisha.

"Kwa masikitiko makubwa natangaza kifo cha kiongozi mkubwa Afrika, Daniel Toroitich arap Moi, rais wa pili wa Kenya. Raisi mstaafu amefariki katika Hospitali ya Nairobi mapema asubuhi ya leo Februari 4 akiwa na familia yake.

Msemaji wa Mzee Moi Lee Njiru pia ameongea na BBC Swahili punde tu taarifa hizo zilipochomoza na kabla ya Ikulu kutoa tamko.

"...alikuwa Nairobi Hospital ambapo alilizwa tarehe 10 mwezi wa kumi mwaka uliopita, hiyo ni zaidi ya miezi mitatu," bwana Njiru amesema.

Kwa mujibu wa Njiru mipango yote ya mazishi ipo chini ya jeshi la Kenya kwa kuwa Mzee Moi alikuwa amiri jeshi mstaafu wa nchi hiyo.

Runinga ya taifa ya Kenya (KBC), pamoja na vyombo binafsi vya Capital FM, Citizen TV na NTV vimeripoti taarifa hiyo ya msiba asubuhi ya leo Jumanne, Februari 4.

Mzee Moi alizaliwa Septemba 2, 1924 na alitawala Kenya kwa miaka 24 kutoka 1978 mpaka 2002.from MICHUZI BLOG https://ift.tt/394B8z1
via
logoblog

Thanks for reading Rais mstaafu wa Kenya Daniel Arap Moi afariki dunia

Previous
« Prev Post