Raia wawili wa Iran wafariki dunia mjini Qom kwa maradhi ya virusi vya Corona

  Masama Blog      
Mkuu wa Kituo cha Mawasiliano ya Umma na Upashaji Habari cha Wizara ya Afya nchini Iran, amethibitisha habari ya kufariki dunia watu wawili kutokana na maambukizi ya virusi vya Corona mjini Qom nchini hapa.

Kiyanush Jahanpur aliyasema hayo jana Jumatano na kubainisha kwamba kufuatia ongezeko la matatizo ya kupumua lililoshuhudiwa katika siku za hivi karibuuni mjini Qom, uchunguzi wa vipimo ulithibitisha kesi mbili za maambukizi ya virusi vya Corona.
 
 Ameongeza kwa kusema: "Kwa bahati mbaya watu wawili ambao ni wazee na kutokana na upungufu wa vifaa vya tiba katika wodi maalumu za hospitali za mji huo, walipoteza maisha yao kwa maradhi hayo." 
 
Wakati huo huo Ali Larijani, Spika wa Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu ya Iran (Bunge) jioni ya jana alizungumza kwa njia ya simu na Waziri wa Afya, Tiba na Mafunzo ya Udaktari wa Iran, Saeed Namaki ambapo sambamba na kumueleza kuwa amepata taarifa za kuthibitika kesi mbili za ugonjwa unaotokana na virusi vya Corona mjini Qom, alitaka kuchukuliwa hatua za dharura kwa ajili ya kuzui na kuwatibu waathirika wa maradhi hayo.
 


from MICHUZI BLOG https://ift.tt/329oHzK
via
logoblog

Thanks for reading Raia wawili wa Iran wafariki dunia mjini Qom kwa maradhi ya virusi vya Corona

Previous
« Prev Post