PROGRAMU YA TANO NA SITA YA MWANAMKE WA WAKATI UJAO YAZINDULIWA

  Masama Blog      
Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii

Chama cha Waajiri Tanzania (ATE) wamezindua programu ya tano na sita kwa wanawake wa wakati ujao ikiwa na ongezeko la washiriki wengi kutoka taasisi na makampuni mbalimbali.

Mafunzo hayo yanaendeshwa ATE kwa kushirikiana na Chuo cha Uongozi cha ESAMI toka mwaka 2016 yakiwa na lengo la kumuandaa mwanamke kushika uongozi wa juu.

Akizungumza na waandishi wa habari baada ya uzinduzi huo, Mkurugenzi Mtendaji wa ATE Dkt Aggrey Mlimuka amesema kwa mwaka huu muitikio wa wanawake umekuwa ni mkubwa sana tofauti na miaka mingine.

Amesema, Kila mwaka wamekuwa na darasa moja la wanafunzi 24 ila kwa mwaka huu wamepata watu wengi zaidi hadi kufikia 48 na kugawa kwenye madarasa mawili.

"Tumekuwa na muitikio mkubwa sana, programu hii imekuwa na mchango mkubwa sana katika taasisi wanazozifanyia kazi na wameweza kuonesha umuhimu wa mwanamke katika uongozi," amesema Dkt Mlimuka.

Aidha, amesema kozi hii imeweza kuwaandaa wanawake katika nyanja tatu ikiwemo katika uongozi wa ngazi mbalimbali wakiwa wameandaliwa vizuri, na mchango wao ukiwa na uhakika na kampuni na wameonesha uhai  na kupelekea makampuni hayo kuona umuhimu wa mafunzo yanayotolewa.

"ATE tumekuwa tunawaandaa katika mambo  mbalimbali ikiwemo Uongozi, wajumbe wa bodi za wakurugenzi na kuwafundisha namna ya kuandaa hotuba na mazungumzo yao,"

Programu ya Mwanamke wa Wakati ujao ilizunduliwa mwaka 2016 na Makamu wa Rais Samia Suluhu na ni mafunzo yanayopewa kipaumbele na serikali katika kumjenga mwanamke wa wakati ujao.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Waajiri Tanzania (ATE) Dkt Aggrey Mlimuka akizungumza na waandishi wa habari baada ya uzinduzi wa programu ya tano na sita ya mafunzo kwa mwanamke wa wakati ujao yenye lengo la kumuandaa mwanamke katika uongozi..

Picha ya pamoja ya washiriki wa programu ya tano na sita ya mafunzo kwa mwanamke wa wakati ujao yenye lengo la kumuandaa mwanamke katika uongozifrom MICHUZI BLOG https://ift.tt/32gNT7u
via
logoblog

Thanks for reading PROGRAMU YA TANO NA SITA YA MWANAMKE WA WAKATI UJAO YAZINDULIWA

Previous
« Prev Post