PINDA AZINDUA KITABU CHA 'MAKING AFRICA WORLD'S LARGEST ECONOMY' KILICHOTUNGWA NA MWANAHABARI NGULI DEREK MURUSURI

  Masama Blog      

NA K-VIS BLOG

Waziri Mkuu Mstaafu na Mkuu wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania, (OUT) Mhe. Mizengo Kayanza Peter Pinda amezindua kitabu cha “MAKING AFRICA WORLD'S LARGEST ECONOMY” kilichoandikwa na mwanahabari nguli na mtaalamu wa masuala ya kiuchumi, Bw. Derek Murusuri.

Kitabu hiki kinashajihisha Waafrika kufikiri na kutekeleza mageuzi endelevu yatakayoifanya Afrika kuwa ni Bara lenye nguvu kubwa ya kiuchumi.

Kwa mujibu wa mtunzi wa kitabu hicho Bw. Derek Murusuri, kabla ya kuandika kitabu hicho alifanya utafiti kwa takriban miaka 21 na kwamba maudhui yaliyomo ndani ya kitabu hicho yataleta mabadiliko katika Afrika ijayo.

Uzinduzi huo umefanyika Januari 29, 2020 jijini Dar es Salaam.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mkuu wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania, (OUT) Mhe. Mizengo Kayanza Peter Pinda, akizunguzma wakati akizundua kitabu cha "MAKING AFRICA WORLD'S LARGEST ECONOMY" jijini Dar es Salaam Januari 29, 2020.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mkuu wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania, (OUT) Mhe. Mizengo Kayanza Peter Pinda, akimpongeza mtunzi wa kitabu hicho, Bw. Derek Murusuri mara baada ya kukizindua.
Balozi Christopher Liundi akizungumza wakati wa hafla hiyo.

Bw. Derek Murusuri akizungumza wakati wa hafla hiyo.
Mtangazaji mkongwe nchini, Bw. Jacob Tesha akitoa nasaha zake.
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano, Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Bw.Frederick Ntobi, akizungumza


from MICHUZI BLOG https://ift.tt/2RP3qYr
via
logoblog

Thanks for reading PINDA AZINDUA KITABU CHA 'MAKING AFRICA WORLD'S LARGEST ECONOMY' KILICHOTUNGWA NA MWANAHABARI NGULI DEREK MURUSURI

Previous
« Prev Post