NMB kuhakikisha Mkoa wa Songwe unakuwa kiuchumi kupitia wawekezaji

  Masama Blog      
WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Uwekezaji - Angela Kairuki amewata wawekezaji wa ndani na nje ya nchi kutumia fursa ya Mkoa wa Songwe kuwa lango la nchi za SADC kwa kwenda kuwekeza katika sekta mbalimbali zilizopo Mkoani humo hasa katika sekta ya Kilimo ili kuinua uchumi wa Mkoa huo na nchi kwa ujumla.

Angela alisema hayo jana wakati alipokuwa akizindua kongamano la uwekezaji Mkoa wa Songwe, lililofanyika katika kiwanja cha Vwawa Wilayani Mbozi. Aliongeza kuwa, Mkoa huo una fursa nyingi ambazo zimeanishwa za biashara na uwekezaji zinazotokana na kuwekwa kimkakati na viongozi wa Mkoa kwa kuwa kiungo kati ya Tanzania na nchi zaidi ya 16 za SADC.

Aidha alisema kuwa, katika suala la uwekezaji Mkoa uhakikishe unatenga meaneo ya uwekezaji katika kila Halmshauri kwa kuweka miundo mbinu mbalimbali ili kumrahisishia mwekezaji pindi anapoenda kuwekeza katika Halmashauri.

Awali akimkaribisha Mgeni rasmi katika kongamano hilo, Mkuu wa Mkoa wa Songwe - Brigedia General Nicodumus Mwangela alisema, Mkoa wa Songwe umeaandaa kongamano lenye lengo la kutangaza fursa na vivutio vya uwekezaji vilivyopo katika Halmashauri zote za Mkoa huo ili kuvutia wawekezaji wa ndani na nje ya nchi.

Aidha, mmoja wa wadhamini wa kongamano hilo Benki ya NMB - Filbert Mponzi ambaye ni Afisa Mkuu wa Wateja Binafsi, Biashara Ndogo na za Kati alisema kuwa Benki yake imetoa jumla ya shilingi bilioni 22 katika Mkoa wa Songwe kwenye sekta ya kilimo hasa katika mazao ya kahawa ,mahindi na mengine yanayolimwa Mkoani humo.

Alisema kuwa, kwa mwaka huu benki hiyo imeanza kufungua akaunti kwa ajili ya wakulima ambapo ni wito wa Serikali kupitia Wizara ya Kilimo kwa wakulima wote lazima walipwe kwenye akaunti zao na kuwa akaunti hizo zitafunguliwa bure ili wakulima wote waingie katika mfumo ambao uko rasmi.

Mponzi alisema kuwa benki ya NMB imeanza kutoa mikopo kwa wajasiliamali yenye riba nafuu lakini hata yenye dhama ambazo siyo rasmi, ikiwa na lengo la kuwawezesha wajasiliamali wadogo wote waweze kunafaika na mikopo ya benki, hivyo hata kufuatia mikopo hiyo wanaimani watatokea wawekezaji wa kati hata wadogo Mkoa Songwe watakaoenda kupata mkopo NMB. Katika uwekezaji wake Benki hiyo imefanikiwa kutoa mikopo ya shilingi bilioni 400 kwa wajasilimali wadogo na wakati..

Mbali na kusaidia wajasiliamali lakini pia benki hiyo imekuwa ikisaidia katika miradi mbalimbali hapa nchini na kuwasaidia wakandali mbalimbali ambapo mpaka sasa wametoa dhamana kwa wakandalia wa ndani zaidi ya mia 400 kupitia uhusiano walionao na TARURA.

Afisa huyo alimuhakikishia Waziri huyo kuwa watashirikiana na Mkoa wa Songwe katika kuhakikisha wawekezaji wanasaidiwa katika benki yao pindi watakapoenda kwa ajili ya kutaka huduma mbalimbali za kifedha ilikwa na lengo la kuhakikisha Mkoa wa Songwe unakuwa kiuchumi kupitia wawekezaji wao.
#NMBKaribuYako
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Uwekezaji Angela Kairuki akimkabidhi cheti maalumu Afisa Mkuu kwa Wateja Binafsi Biashara Ndogo na za Kati wa NMB - Filbert Mponzi wakati wa Kongamano la Uwekezaji lililofanyika katika viwanja vya Vwawa Mkoani Songwe.from MICHUZI BLOG https://ift.tt/2P1tTQZ
via
logoblog

Thanks for reading NMB kuhakikisha Mkoa wa Songwe unakuwa kiuchumi kupitia wawekezaji

Previous
« Prev Post