NACTE YAVIFUNGIA VYUO 10 KWA KUTOKIDHI VIGEZO, TSJ NACHO

  Masama Blog      
VYUO vya elimu ya ufundi 10 vimefutiwa usajili ikiwa ni matokeo ya ukaguzi wa vyuo 105 uliofanyika kati ya Oktoba na Desemba, 2019 na kubaini kuwa vyuo hivyo havikidhi vigezo vya kutoa mafunzo yanayoratibiwa na Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE).

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar ea Salaam leo,Mkurugenzi wa uthibiti, Ufatiliaji na Tathimini, katika Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi, Dkt.Jofrey Oleke amesema kuwa vyuo vilivyofungiwa kutokana na sababu mbalimbali.

Vyuo vilivyofungiwa ni ERA Training College- kilichosajili 2015 kipo Bukoba, Azania College of Management kimesejiliwa 2009 kipo Dar es Salaam, Time School of Journalism, Clever College kimesajiliwa 2007, kipo Dar es Salaam, Aces College of Economic Sciences (ACES) Mwanakwerekwe Zanzibar.

Zanzibar Institute of Business Research and Technology (ZIBRET)-Mwanakwerekwe Zanzibar kimesajiliwa 2015 na Gender Trainning Institute-Dar es Salaam kilochosajiliwa  2009.

Vyuo vingine ni College of Business Management -Dar es Salaam kilichosajiliwa 2014 na University Computing Centre (UCC), Mwanza Cumpus kilichosajiliwa 2009.

Amesema kuwa Baraza limevifutia usajili vyuo hivyo baada ya kubaini mapungufu mbalimbali aidha kabla ya kuvitutia usajili vyuo hivyo baraza lilibiandikia barua ili kuhakikisha vinarekebisha changamoto walizozibaini wakati wa ukaguzi.

"Baraza limevitaarifu vyuo husika kwa barua juu ya maamuzi ya kuvifuyoa usajili na kuvutaka Vihakikishe kuwa wanafunzi wote waliosajiliwa katika mfimo wa udahili wa baraza wanahamishwa mara moja kwendavyuo vingine vilivyosajiliwa." Amesema Dkt. Oleke.

Hata hivyo vyuo hivyoo havikutii maagizo halali ya Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE).

Kwa upande  wa Mkurugenzi Malezi na Ushauri wa vyuo vya ufunzi (NACTE), Mhandisi Dkt. Gemima Modu amesema vyuo vilivyojiunga na chuo kikuu cha Zanzibar ni Chuo cha Kilimo cha Zanzibar.

"Uamuzi huo umefikiwa kwa kuzingatia kifungu cha 20 (1) cha kanuni za isajili wa vyuo vya elimu ya ufundi 2001 (GN 279 of 26/10/2001)".Amesema Mhandisi Dkt Gemima.

Hata hivyo moja ya Mwanafunzi wa chuo kimojawapo ya vilivyofungiwa amesema kuwa amesikitishwa na uamuzi huo na anaomba ni mchakato wa kuhamishiwa kwenye vyuo vingine usichukue muda mwingi ili wanafunzi wanaoendele na masomo waweze kuendelea.


from MICHUZI BLOG https://ift.tt/39iFYZu
via
logoblog

Thanks for reading NACTE YAVIFUNGIA VYUO 10 KWA KUTOKIDHI VIGEZO, TSJ NACHO

Previous
« Prev Post