MITANDAO YA KIJAMII YAZIDI KUONGEZA WIGO WA AJIRA KWA VIJANA,'APP' YA BIDHAA YA KEKI YAZINDULIWA LEO JIJINI DAR

  Masama Blog      
Mitandao ya kijamii   imeongeza wigo katika ajira kwa vijana kufanya ubunifu mbalimbali ikiwemo uuzaji wa bidhaa kwa kutumia mitandao hiyo.

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Melisa Lilian Ringo wakati akizindua App kwa ajili ya Keki iliyofanyika leo, jijini Dar es Salaam.

Ringo amesema kuwa watu wanaohitaji Keki watakwenda kwenye mtandao na kufungua 'Melisa Cake'  na kuchagua aina mbalimbali za Keki.Amesema mteja akiingia katika App hiyo atachagua Keki aitakayo baada ya hapo  Kampuni itapeleka keki moja kwa moja kwa mteja .

Ringo amesema wanatengeneza keki za matukio mbalimbali na  bei zake kila mtanzania  anaweza kumudu.

Aidha amesema kuwa licha ya kutengeneza keki wanauza vifaa vya kutengeneza Keki pamoja na kuwapo kwa madarasa ya kutengeneza Keki."Tanzania ya Viwanda tuitumie kwa kutengeneza vitu mbalimbali vinavyotuzunguka kutokana na mahitaji ya kiwanda, sio lazima uwe na mtambo mkubwa"amesema Ringo.

Hata hivyo amesema kuwa bidhaa ya Keki ipo lakini sasa watakwenda kisasa kwa kutumia mitandao kuzungumza gharama ya kutoka sehemu Mmoja kwenda nyingine.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Melisa Lilian Ringo akionesha Aina ya Keki waliotengeneza kwa ajili ya uzinduzi katika hafla iliyofanyika jijini Dar es Salaam.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Melisa Lilian Ringo akikata keki mara baada ya uzinduzi wa App ya Melisa Cake iliyofanyika jijini Dar es Salaam
 Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Melisa  Lilian Ringo akizungumza na waandishi habari kuhusiana na uzinduzi wa App kwa ajili ya uuzaji wa Keki katika mtandao kwa kufungua Melisa Keki,jijini Dar es Salaam.


from MICHUZI BLOG https://ift.tt/2T8QhJ8
via
logoblog

Thanks for reading MITANDAO YA KIJAMII YAZIDI KUONGEZA WIGO WA AJIRA KWA VIJANA,'APP' YA BIDHAA YA KEKI YAZINDULIWA LEO JIJINI DAR

Previous
« Prev Post