MHANDISI MSOMI AIBUKA KINARA SHINDANO LA MISS UTALII DAR ES SALAAM 2020

  Masama Blog      
Matunda ya muundo mpya wa uongozi na shindano, pia kanuni na taratibu mpya za shindano la Miss Utalii Tanzania, uliopitishwa na serikali kupitia Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) yameanza kuonekana, kwa wasomi kutoka katika vyuo vikuu mbalimbali na wahitimu wa vyuo mbalimbali kujitokeza kuwania mataji katika ngazi mbalimbali za shindano hilo.
 Katika udahili (Auditions) ya kupata washindi wa Miss Utalii Dar Es Salaam na wilaya zake mwaka 2020,watakao wakilisha mkoa wa Dar Es Salaam ,katika fainali za Miss Utalii Ukanda wa Pwani ya Kaskazini 2020 (Miss Tourism North Cost Circuit 2020),ukanda unao undwa na mikoa ya Dar Es Salaam,Tanga na Pwani,tulishudia zaidi ya washiriki 40 kati ya zaidi ya 100 walio omba kushiriki wakiwa wametimiza sharti la viwango vya elimu.
Katika mchuano huo ulio tanguliwa na semina ya washiriki ulifanyika ,Jumamosi ya Tarehe 15-2-2020,katika hoteli ya kitalii ya Jaromax Palace ,iliyopo Tiptop Dar Es Salaam, Mhandisi Msomi,Sarafina Mwirabi Mhitimuwa Chuo cha Ufundi Arusha, na Mwanafunzi  wa Mwaka wa Pili   wa Degree ya Oil and Gas katika chuo DIT Dar es Salaam,ambaye pia ni Miss Utalii Kinondoni 2020  aliibuka  mshindi wa Taji la Miss Utalii Dar Es Salaam 2020,akiwashinda washiriki wengine zaidi ya 40 kutoka wilaya zote za Dar Es Salaam.
Mshindi wa pili wa Miss Utalii Dar Es Salaam 2020, ni Jane Jayambo wa chuo kikuu cha Dar Es Salaam,ambaye pia ni Miss Utalii Temeke 2020, ,Mshindi wa tatu ni Paulina Allute wa chuo cha DIT, ambaye pia ni Miss Utalii Ubungo 2020,wa nne ni Jasmini wakullu wa chuo cha Mwalimu Nyerere, ambaye pia  Miss Utalii Kigamboni 2020,na wa tano ni Falha Maulidi  wa chuo cha DSJ ambaye pia ni Miss Utalii Kinondoni 2020.
 Washirikin wengine ambao waliingia katika ishirini bora ni Amina Juma wa chuo kikuu cha Dar Es Salaam na Janeth Mgweno toka Ubungo,Diana John wa chuo kikuu cha Dar Es Salaam na Clemencia Method mhitimu wa chuo cha afya na ukunga Dar Es Salaam toka wilaya Kinondoni,Witness Romanus na Bertha Kakete wa chuo kikuu cha Dar Es Salaam toka wilaya ya Ilala,Doris Barnabas wa chuo kikuu cha kodi na Rose Kauzeni wa chuo kikuu cha Dar Es Salaam toka wilaya ya Kigamboni.
Washindi hawa watawakilisha mkoa wa Dar Es salaam katika fainali ya kumpata Miss Utalii Kanda ya Pwani ya kaskazini 2020(Miss Tourism North cost 2020) inayo jumuisha washindi kutoka mikoa ya Dar Es Salaam,Tanga na Pwani.


from MICHUZI BLOG https://ift.tt/2vMx0oS
via
logoblog

Thanks for reading MHANDISI MSOMI AIBUKA KINARA SHINDANO LA MISS UTALII DAR ES SALAAM 2020

Previous
« Prev Post