MASHIRIKA, TAASISI NA ASASI ZA KIRAIA WAASWA KUCHANGAMKIA FURSA ZITAKAZOJITOKEZA KATIKA UCHAGUZI WA MKUU WA 2020

  Masama Blog      
Na Avila Kakingo, Globu ya Jamii
MASHIRIKA na Asasi za kiraia hapa nchini wahimizwa kuchangamkia fursa zitakazojitokeza katika uchaguzi Mkuu wa 2020.

Aidha Mashirika na Asasi za kiraia hizo wanaotaka kutoa elimu ya mpigakura kwa jamii wajitokeze kutuma maombi Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC).

Hayo ameyasema Mkurugenzi Mtendaji wa Asasi za Kiraia, Francis Kimwanga jijini Dar es Salaam leo, wakati wa mkutano na viongozi wa Asasi za kiraia na kuangalia wajibu wa asasi za kiraia katika uchaguzi wa kidemokrasi hapa nchimi.

" Ni vizuri kila Mwananchi katika uchaguzi Mkuu mwenye sifa anatakiwa kupiga kura kwa amani ili amchague kiongozi anayemtaka kwaajili ya kumuongoza kwa miaka mitano ijayo".

Amesema kuwa mazungumzo ya leo yatawawezeshe Asasi za kiraia na mashirika kutoa elimu kwa kila mwananchi kushiriki katika uchaguzi mkuu wa 2020.

Kwa Upande wa Mwenyekiti wa Baraza la Taasisi zisizo za kiserikali(NGO's), Nichorus Zacharia amesema mikakati yao kama Asasi za kiraia ni kuangalia namna ambavyo wanaweza kuboresha na kuongeza ushiriki wa wananchi katika uchaguzi Mkuu wa 2020.

"Jukuwaa hili ni huru na kila Asasi ya kiraia inaweza kutoa maoni yake kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka huu na kila mwezi kutakuwa na majukwaa tofauti kwaajili ya kuzungumzia mambo ya uchaguzi na mambo mengine". Amesema Zacharia

Zacharia amesema kuwa matamanio yao ni uchaguzi mkuu uwe wa haki na amani ili kiongozi atakaye patikana aweze kutuongoza kwa kipindi hicho.

Hata hivyo Mwanasheria wa Tume ya Taifa ya uchaguzi(NEC), Emmanuel Kawishe amesema kuwa Tume ya Taifa ya uchaguzi katika uboreshaji wa daftari la kudumu la mpiga kura kwa mikoa yote ya Tanzania bara na Zanzibar imeshakamilika kwa awamu ya kwanza bado mikoa mitatu tuu na Morogoro ndio wanamalizia.

"Elimu ya mpiga kura imetolewa ya kutosha na wananchi wamejitokeza kwa kiasi kikubwa, watu wapo huru kujiandikisha na mpaka sasa". Amesema Kawishe.

Amesema kuwa baadhi ya wananchi wakati wa uboreshaji wa Daftari la kudumu la mpiga kura wanakuwa kwenye shughuli za kilimo ambapo wanaleta mrundikano kwa siku za mwisho, sasa tume itarudi kwa mara ya pili ili kuhakikisha kila mwananchi anajiandikisha katika daftari ya kudumu la mpiga kura kwa wale ambao hawakujiandikisha.
Mkurugenzi Mtendaji wa Asasi za Kiraia, Francis Kimwanga akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo wakati wa mkutano na viongozi wa Asasi na mashirika ya Kiraia wakijadili mchango wa Asasi za kiraia katika uchaguzi wa Kidemokrasia hapa nchini.
Mwenyekiti wa Baraza la Taasisi zisizo za kiserikali(NGO's), Nichorus Zacharia akizungumza na waandishi wa habari jinini Dar es Salaam leo, wakati wa kikao cha Viongozi wa Asasi za Kiraia na Mashirika hapa nchini na kujua mchango wa asasi hizo katika uchaguzi wa Kidemokrsia hapa nchini.
Mwanasheria wa Tume ya Taifa ya uchaguzi(NEC), Emmanuel Kawishe akizungumza na waandishi wa habari jinini Dar es Salaam leo, wakati wa kikao cha Viongozi wa Asasi za Kiraia na Mashirika hapa nchini na kujua mchango wa asasi hizo katika uchaguzi wa Kidemokrsia hapa nchini.
Mkurugenzi Mtendaji wa Asasi za Kiraia, Francis Kimwanga akizungumza na viongozi wa Asasi za kiraia na mashirika jinini Dar es Salaam leo, wakati wa kikao cha Viongozi wa Asasi za Kiraia na Mashirika hapa nchini na kujua mchango wa asasi hizo katika uchaguzi wa Kidemokrsia hapa nchini.Baadhi ya vingozi wa Taasisi, shirika na Asasi za Kiraia wakisikiliza kwa Lugha ya Alama.


Baadhi ya washiriki wakizungumza na viongozi wa taasisi, Asasi na mashirika ya kiraia leo wakati wakiangalia wajibu wa Asasi hizo katika uchaguzi wa Kidemokrasia.


from MICHUZI BLOG https://ift.tt/3bhIVvi
via
logoblog

Thanks for reading MASHIRIKA, TAASISI NA ASASI ZA KIRAIA WAASWA KUCHANGAMKIA FURSA ZITAKAZOJITOKEZA KATIKA UCHAGUZI WA MKUU WA 2020

Previous
« Prev Post