MASAUNI ATEMBELEA CHUO CHA ZIMAMOTO NA UOKOAJI CHOGO NA KUFANYA MKUTANO NA WAKIMBIZI RAIA WANAOLALAMIKIA KUPORWA ARDHI

  Masama Blog      
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,Mhandisi Hamad Masauni akimsikiliza Mkuu wa Chuo cha Zimamoto na Uokoaji Chogo ,Kamishna Msaidizi,Kennedy Komba(kulia) wakati wa ukaguzi wa mabweni yanayotumiwa na wanafunzi wa chuo hicho kilichopo wilayani Handeni mkoani Tanga,leo.Katikati ni Mkuu wa Wilaya ya Handeni Godwin Gondwe.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,Mhandisi Hamad Masauni(wapili kulia),Mkuu wa Wilaya ya Handeni,Godwin Gondwe (watatu kulia),Mbunge wa Handeni Vijijini,Mboni Mhita(kushoto) na   Mkuu wa Chuo cha Zimamoto na Uokoaji Chogo ,Kamishna Msaidizi,Kennedy Komba(kulia), wakipita katika moja ya mabweni yanayojengwa katika chuo wakati wa ziara ya naibu waziri leo kukagua ujenzi  wa mabweni  wilayani Handeni mkoani Tanga.
Mkuu wa Wilaya ya Handeni, Godwin Gondwe akizungumza na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni(hayupo pichani),wakati wa kikao cha ndani kilichohusisha Wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama baada ya naibu waziri kuwasili wilayani Handeni leo  kwa ziara ya kikazi.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akisalimiana na viongozi wa wilaya ya Handeni,mkoani Tanga leo baada ya kuwasili katika kijiji cha Chogo kwa ziara ya kikazi.Kushoto ni Mkuu wa wilaya hiyo,Godwin Gondwe.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi


from MICHUZI BLOG https://ift.tt/31SR8Sp
via
logoblog

Thanks for reading MASAUNI ATEMBELEA CHUO CHA ZIMAMOTO NA UOKOAJI CHOGO NA KUFANYA MKUTANO NA WAKIMBIZI RAIA WANAOLALAMIKIA KUPORWA ARDHI

Previous
« Prev Post