Mafia Yamshukuru Rais Magufuli kwa Kupata Mawasiliano ya simu kijijini Chunguruma

  Masama Blog      
Serikali imejenga mnara wa Mawasiliano Kijiji Cha Chunguruma, Ndagoni Mafia, ambapo kwa mara ya kwanza wananchi wanapata mawasiliano. 

 Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Mh. Injinia Atashasta Nditiye amezindua mnara  huo wa Mawasiliano kwa kijiji cha Chunguruma kilichoko Kata ya Ndagoni Wilaya ya Mafia. Kijiji hicho na maeneo jirani havikuwa na usikivu wa Mawasiliano ya simu Za mkononi kwa muda mrefu.

 Akizungumza katika uzinduzi huo, Mbunge wa Wilaya ya Mafia, Mheshimiwa Mbaraka Dau, ameiashukuru Serikali ya Awamu ya Tano kwa kutimiza ahadi ya kuhakikisha kijiji hicho na maeneo jirani yanapata huduma Za mawasiliano ya simu Za mkononi. 
 “Nakushukuru sana Mh. Naibu Waziri kwa kutimiza ahadi ya Serikali kuleta mawasiliano Chunguruma, tufikishie salamu za wananchi wa Mafia kwa Mh. Rais wetu Kipenzi John Pombe Joseph Magufuli kwa kutuletea maendeleo ya Mawasiliano Mafia” alisema Mh. Dau. 
Mheshimiwa Nditiye akijibu salamu hizo, alisema Serikali ya Awamu ya Tano inatambua kuwa mawasiliano ni haki ya wananchi na katika Ilani ya Uchaguzi ya CCM iliahidi kuhakikisha kila mtanzania anapata mawasiliano. 
 “Mheshimiwa Rais John Pombe Joseph Magufuli anataka kuona Watanzania wote wanapata huduma Za mawasiliano kote nchini. Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano kupitia Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote hatu laki usingizi ili kukamilisha kazi hii. Mimi jukumu langu ni kuhakikisha wananchi wote wanapata huduma za simu kwa Mawasiliano na huduma za kutuma na kupokea miamala ya fedha na kufanya malipo kupitia teknolojia ya mawasiliano”, alisema Mheshimiwa Nditiye. 
 Mwaka jana 2019 mwezi wa tano, Mh Nditiye alifanya ukaguzi wa usikivu was huduma Za mawasiliano na kubaini eneo la Chunguruma halikuwa na huduma ya mawasiliano. Aliuagiza Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) kujenga mnara kwa kushirikiana na kampuni ya simu. @vodacomtanzania ilishinda tends ya kujenga mnara huo wenye 3 G na umeanza kufanya kazi, na wananchi wa maeneo ya Ndagoni na maeneo ya jirani. 
 Awali Mkuu wa Wilaya hiyo Mheshimiwa Shaib Mnunduma aliishukuru Serikali kwa kujenga mnara huo ambao utasaidia wananchi kuwasiliana na kupata huduma Za dharura hasa wavuvi wanapokuwa baharini. 
 Akizungumza na wananchi wa Chunguruma, Mtendaji Mkuu wa Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote Bibi Justina Mashiba amewahakikishia viongozi na wananchi wa Wilaya ya Mafia kuwa changamoto za mawasiliano katika Wilaya ya Mafia zitaisha na kwa sasa Serikali kupitia Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote Una miradi ya kujenga minara 5 ya Mawasiliano katika Wilaya hiyo hivi karibuni. 

Mnara wenye kasi ya 3G uliojengwa na Serikali kwa kutoa ruzuku kwa Vodacom uliojengwa katika kijiji cha Chunguruna kata ya Ndagoni Wilaya ya Mafia.
Sent from my iPhone


Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Mheshimiwa Atashasta Nditiye akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Chunguruma, Ndagoni Mafia alipokwenda kuzindua mnara wa Mawasiliano uliojengwa na Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF)

Wananchi wa Kijiji cha Chunguruma kilichoko Kata ya Ndagoni wakimsikiliza Naibu Waziri Mh. Atashasta Nditiye (Mb) wakati wa uzinduzi wa mnara wa Mawasiliano kijijini hapo.

Wananchi wa Kijiji cha Chunguruma kilichoko Kata ya Ndagoni wakimsikiliza Naibu Waziri Mh. Atashasta Nditiye (Mb) wakati wa uzinduzi wa mnara wa Mawasiliano kijijini hapo.

Mkuu wa Wilaya ya Mafia Mh. Shaib Mnunduma akimshukuru Mh. Naibu Waziri wa Uchukuzi na  Mawasiliano kwa kutimiza ahadi ya kujengwa kwa Mnara wa Mawasiliano kijijini Chunguruma kata ya Ndagoni Mafia alipotembelea Wilaya hiyo mwezi Mei 2019. Mnara huo uliojengwa na Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote kwa kutoa ruzuku kwa VODACOM umezinduliwa Jumamosi tarehe 1, 2020.

Mkuu wa Wilaya ya Mafia Mh. Shaib Mnunduma akimshukuru Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Mheshimiwa Atashasta Nditiye kwa kujengwa kwa Mnara wa Mawasiliano kijijini Chunguruma kata ya Ndagoni Mafia. Anayeshuhudia ni Naibu Katibu Mkuu Mawasiliano Dr. Jim Yonazi na mjumbe wa Bodi ya UCSAF Bibi Eunice Masigati

Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Mheshimiwa Atashasta Nditiye akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Chunguruma, Ndagoni Mafia alipokwenda kuzindua mnara wa Mawasiliano uliojengwa na Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF)from MICHUZI BLOG https://ift.tt/37RIK7I
via
logoblog

Thanks for reading Mafia Yamshukuru Rais Magufuli kwa Kupata Mawasiliano ya simu kijijini Chunguruma

Previous
« Prev Post