DOWNLOAD APP YETU HAPA

Maandalizi ya mazishi ya Rais mstaafu Daniel Arap Moi yanaendelea

  Masama Blog      
Zaidi ya watu 10,000 wanatarajiwa kuhudhuria mazishi ya rais mstaafu Daniel Arap Moi siku ya Jumatano.

Ibada ya wafu ya kumuaga mzee Daniel Arap Moi inafanyika katika uwanja wa kitaifa wa michezo wa Nyayo na inatarajiwa kuanza saa nne asubuhi 
 
.Mahema yanaendelea kuwekwa katika shule ya Kabarak huku shughuli zingine za matayarisho zikiendelea


Mwili wa aliyekuwa rais unatarajiwa kuwasili katika uwanja huu Jumatano asubuhi ukitokea Nairobi ,Marais 18 kutoka mataifa mbalimbali wanatarajiwa kuhudhuria ibada ya kumuaga rais mstaafu Daniel Arap Moi,Waombolezaji 30,000 wanatarajiwa kuhudhuria ibada ya kumuaga Daniel Toroitich Arap Moi


Shughuli ya mazishi itasimamiwa na jeshi la taifa, na kuongozwa na kanisa la African Inland Church.

Ni familia pekee watakaoruhisiwa kushuhudia mazishi huku raia wakiwa wamepata fursa ya kutoa heshima zao za mwisho kwa siku tatu. Serikali imetoa hakikisho kwamba maandalizi ya mazishi ya Daniel Arap Moi yanaendelea vyema

Raia na wageni wengine watahudhuria ibada lakini hawataruhusiwa kwenye mazishi yenyewe. 
 
HABARI PICHA KWA HISANI YA BBC Swahili.
from MICHUZI BLOG https://ift.tt/2SjMD0d
via
logoblog

Thanks for reading Maandalizi ya mazishi ya Rais mstaafu Daniel Arap Moi yanaendelea

Previous
« Prev Post