LUKUVI KUTEKELEZA AGIZO LA RAIS KURUDISHA UMILIKI WA EKARI 750 MANISAPAA YA KIGAMBONI JUMATATU IJAYO

  Masama Blog      
Na Munir Shemweta, WANMM DODOMA
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi Jumatatu tarehe 17 Februari 2020 atakwenda katika halmashauri ya Manispaa ya Kigamboni kwa ajili ya kurudisha umiliki wa ekari 750 kwa manispaa hiyo kama ilivyoelekezwa na Rais Magufuli.
Rais John Pombe Magufuli alitoa siku saba kuanzia jumanne iliyopita kwa Wizara ya Ardhi kurejesha miliki ya eneo hilo kwa Halmashauri ya wilaya ya Kigamboni kufuatia kufuta miliki ya eneo hilo ili kuwa chini ya Serikali.
Uamuzi wa Lukuvi ni utekelezaji wa agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania John Pombe Magufuli alilolitoa jumanne wiki hii baada ya kuzindua jengo la Manispaa ya Kigamboni na lile la Mkuu wa Wilaya hiyo yaliyoko eneo la Gezaulole jijini Dar es Salaam.
Akizungumza kwa njia ya Mtandao leo tarehe 13 Februari 2020 akiwa Abu Dhabi, Falme za Kiarabu anakohudhuria  Kikao cha Mawaziri wa Afrika Kuhusu Masuala ya Nyumba na Maendeleo ya Miji Lukuvi alisema, jumatatu atakuwa ofisi za Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Kigamboni kwa ajili ya kutekeleza agizo la Rais kuhusiana na urejeshaji miliki ya ardhi kwa halmashauri hiyo.
‘’Jumatatu tarehe 17 Februari 2020 saa tano asubuhi nitakuwa ofisi za Mkurugenzi wa Manispaa ya Kigamboni kwa ajili ya kutekeleza agizo la mhe Rais la kukabidhi ardhi ambayo iko katika eneo la Kigamboni’’ alisema Lukuvi
Kwa mujibu wa Rais Magufuli, pamoja na kufuta umiliki wa eneo hilo ili kuwa chini ya Serikali  lakini umiliki wake haujarerejeshwa


from MICHUZI BLOG https://ift.tt/2Hmhbbf
via
logoblog

Thanks for reading LUKUVI KUTEKELEZA AGIZO LA RAIS KURUDISHA UMILIKI WA EKARI 750 MANISAPAA YA KIGAMBONI JUMATATU IJAYO

Previous
« Prev Post