KLABU YA WYDAD CASABLANCA YA MOROCCO YAMTIMUA KOCHA WAKE MKUU.

  Masama Blog      
Na Yassir Simba, Michuzi Tv.

Klabu ya Wydad Casablanca ya nchini Morocco imemtimua kazi kocha wake mkuu Sebastian Desabre mwezi mmoja tu tangu imteue kushika nafasi hiyo.

Kocha huyo amefutwa kazi mara baada ya klabu ya Wydad Casablanca kupoteza mchezo wake wa ligi weekend iliyopita dhidi ya klabu ya Eljadida kwa bao pekee la winga wa kimataifa wa Tanzania Simon Msuva. Bao hilo pekee na la ushindi katika mchezo huo lilitosha kuotesha nyasi kibarua cha kocha huyo.

Sebastian Desabre ameandamwa na bundi mara ya pili mfululizo katika kibarua chake ndani ya msimu huu mara baada ya hapo awali kutimuliwa katika klabu ya Pyramids inayoshiriki ligii kuu ya nchini Misri.
 


from MICHUZI BLOG https://ift.tt/2P0jaWS
via
logoblog

Thanks for reading KLABU YA WYDAD CASABLANCA YA MOROCCO YAMTIMUA KOCHA WAKE MKUU.

Previous
« Prev Post