KATIBU MKUU KADIO AWATAKA WAKUU WA IDARA WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI KUTATUA CHANGAMOTO ZILIZOPO KWA UMOJA, KAILIMA AMKABIDHI OFISI JIJINI DODOMA LEO

  Masama Blog      
  Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Christopher Kadio akikabidhiwa vitendea kazi vya ofisi hiyo na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Ramadan's Kahilima leo jijini Dodoma.
Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Christopher Kadio akizungumza na watendaji wa wizara hiyo baada ya kuwasili ofisini hapo leo kwa mara ya kwanza yangu ateuliwe na Mhe Rais Dk John Magufuli

 Na Mwandishi Wetu, MOHA, Dodoma. 
KATIBU Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Christopher Kadio, amewataka Wakuu wa Idara na Vitengo wa Wizara yake wafanye kazi kwa ushirikiano na wawe wazi ili kuondoa changamoto mbalimbali zilizopo ndani ya Wizara hiyo. 

Akizungumza baada ya makabidhiano ya ofisi kati yake na aliyekuwa Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Ramadhani Kailima, yaliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Wizara hiyo jijini Dodoma, leo, Katibu Mkuu Kadio amewataka viongozi hao kufanya kazi kwa pamoja na kuwa wazi ili kuiletea Wizara na Serikali kwa ujumla mafanikio chanya.  

“Nashukuru kwa kunikaribisha, nimefurahi kuwa nanyi, ila tufanye kazi kwa mashauriano kwa pamoja, ili tuweze kutatua changamoto mbalimbali ambazo kila Wizara wanazo, na pia nasi tunazo, “ alisema Kadio. 

Pia Kadio alielekeza kuonana na kila Mkuu wa Idara na Kitengo baada ya makabidhiano hayo, ili kusikiliza majukumu yao, pamoja na kujua changamoto mbalimbali zinazowakabili na kutafuta njia ya kuzitafua.

“Nataka mje tuzungumza, kila mmoja wenu aje ofisini kwangu tuzungumze, na pia muwe wazi, muwe wakweli ili nijue majukumu yenu, changamoto zenu ili tuweze kusaidiana,” alisema Kadio. 

Katibu Mkuu Kadio pia aliwapongeza kwa kazi nzuri ambazo Wizara imekuwa inazifanya kwa kipindi chote na kupitia utendaji huo mzuri kuna maboresho na mafanikio ya mambo mbalimbali ndani ya Wizara.

“Nawapongeza kwa kazi nzuri mnazozifanya licha ya kuwepo kwa changamoto lakini tutapambana nazo, kuna maboresho na mmefanikiwa mambo mengi na bado tuna fursa ya kufanya mazuri zaidi,” alisema Kadio. 

Pia Kadio alisema anapenda kila kiongozi kuwa wazi, na kusema yoyote bila woga kwasababu anataka ukweli katika utendaji wake wa kazi.


from MICHUZI BLOG https://ift.tt/2OsIaG7
via
logoblog

Thanks for reading KATIBU MKUU KADIO AWATAKA WAKUU WA IDARA WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI KUTATUA CHANGAMOTO ZILIZOPO KWA UMOJA, KAILIMA AMKABIDHI OFISI JIJINI DODOMA LEO

Previous
« Prev Post