KAMPUNI YA MAFUTA YA PUMA TANZANIA YATOA TUZO, ZAWADI KWA WAENDESHA VITUO VYA MAFUTA NCHINI

  Masama Blog      
KAMPUNI namba moja ya Mafuta Tanzania Puma Energy Tanzania imetoa zawadi kwa waendesha vituo vya mafuta vya Puma vilivyopo nchi nzima ambapo mgeni rasmi Waziri wa Nishati Dk.Merdard Kalemani ametoa pongezi kwa kampuni hiyo kwa namna ambavyo imeendelea kujiimarisha katika utoaji wa huduma za mafuta nchi nchini.

Wakati wa utoaji wa tuzo na zawadi kwa washindi, pia wageni waalikwa mbalimbali walihudhuria wakiwemo maofisa wa Serikali, Kamishna wa Mafuta na Gesi kutoka Wizara ya Nishati, viongozi wa PBPA, EWURA, TAA, OFISI YA MSAJILI WA HAZINA na wengineo. Shughuli ya utoaji wa zawadi na tuzo hizo imetanguliwa na mafunzo ya week nzima yanayowawezesha waendesha vituo hao kufanya kazi kwa ufanisi, weledi, na usalama huku wakihakisha wateja wa mafuta katika vituo vya mafuta vya Puma wanapata huduma bora na za kiwango muda wote.

Akizungumza katika sherehe hizo Mkurugenzi Mkuu wa Puma Bwana Dominic Dhanah amesema, hizi ni tuzo za kwanza za aina yake kufanyika hapa nchini Tanzania ambapo kampuni ya Puma Energy inatambua mchango na kutoa zawadi kwa waendesha vituo bora Zaidi vya mafuta vya Puma Energy. Lengo la tuzo hizi ni kutoa hamasa na kuwapa changamoto waendesha vituo hawa kutoa huduma bora Zaidi kwa wateja wetu kote nchini.

Dhanah akaongeza kwamba Kampuni ya Puma inaunga mkono juhudi za Serikali za kutoa ajira kwa Watanzania na ndio maana inawapa fursa watanzania kuendesha vituo hivi na wao kuajiri watanzania wengine kama wauza mafuta, waendesha maduka , walinzi n.k.Dhanah amesisitiza kuwa Kampuni ya Puma itaendelea kuwajengea uwezo waendesha vituo hawa ili waweze kutoa huduma bora zaidi kwa watanzania.

Akifafanua zaidi tuzo ambazo wamezitoa, amesema ni Muendesha kituo Bora wa Mwaka , Mhudumu bora katika vituo vya mafuta, Kituo chenye Huduma bora kwa wateja kwa huduma tofauti na uuzaji wa mafuta, Muendesha kituo bora wa mwaka kwa huduma za malipo kidijatali, Muendesha kituo bora wa mwaka kwa mahusiano bora na jamii inayomzunguka, Muendesha kituo bora wa mwaka katika ubunifu, Mendesha kituo bora wa mwaka kwa kufuata sheria na miaongozo ya uendeshaji kituo cha mafuta na Muendesha kituo bora katika huduma za Magar na Msimamizi bora wa kituo.

Kwa upande wake Mgeni Rasmi Waziri wa Nishati Medard Kaelamani paomoja na kuwapongeza kampuni ya Puma kwa tukio hilo la kutoa zawadi kwa waendesha vituo wa mafuta, amewasihi waendelee kuwajenga uwezo wa kutoa huduma bora zaidi kwa watanzania.

Waziri Kalemani amesisitiza pia Puma ni kampuni ya Serikali kwa asilimia 50, hivyo ni muhimu ikaongeza wigo wa biashara ku cover maeneo mbali mbali ya nchi ikiwemo vijijini ambako watanzania wengi wanaishi ili kuweza kuongeza mapatao zaidi kwa kampuni, kodi na gawio kwa Serikali lakini zaidi kusogeza karibu zaidi huduma kwa wananchi walio wengi.

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Puma Energy, Dkt. Selemani Majige amemshukuru sana Mheshimiwa Waziri kwa kukubali Mualiko wa Kampuni ya Puma na kushiriki katika sherehe hii, Bodi na Menejimenti tumepokea sifa na changamoto zote ulizo zeieleza hapa na tuna ahidi kuzifanyia kazi ili kuhakikisha kampuni inazidi kufanya vizuri zaidi na kuchangia zaidi katika pato la serikali kwa kodi na gawio.

Akiwapongeza washindi wa tuzo zilizo tolewa Dkt. Majige ame waasa waendesha vituo hao kuongeza weledi zaidi na kuzingatia mafunzo yote waliyo patiwa katika wiki nzima walio kuwa Dar es Salaam na kuhakikisha huduma vituoni zinakuwa zenye tija na bora zaidi kwa wateja.

Kuhusu kampuni hiyo ni kwambaPuma Energy Tanzania ni kampuni ya mafuta iliyosajiliwa ndani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Kampuni inamilikiwa kwa pamoja na serikali ya Jamhuri ya Muungano (Kupitia Msajili wa Hazina, Wizara ya Fedha) pamoja na Puma Investments Limited, kila moja ikiwa na umiliki wa hisa kwa asilimia 50. Kampuni ya Puma ni ya mkondo wa kati kimataifa katika masula ya mafuta na pia kampuni ya mafuta inayojihusisha na uhifadhi mkubwa na usambazaji.

Majukumu makuu ya kampuni ni masoko na usambazaji wa bidhaa za petroli ndani ya Tanzania. Kampuni inauwezo wa kuhifadhi jumla ya lita za mafuta 94 milion, vituo 52 vya mafuta maeneo mbalimbali nchini na inahudumia viwanja vinane vya ndege.
WASHINDI wa tuzo mbalimbali wakiwa katika picha ya pamoja na Waziri wa Nishati, Dk. Medard Kalemani na viongozi wa Kampuni ya Puma Energy Tanzania, wakati wa tuzo za waendesha vituo vya mafuta vya Kampuni ya Puma Energy Tanzania Ltd.

WAZIRI wa Nishati, Dk. Medard Kalemani, akikabidhi tuzo kwa Mkurugenzi wa kituo cha mafuta Puma Arusha Centre, Husein Sajan, baada ya kuibuka mshindi wa kwanza katika tuzo za waqendesha vituo vya mafuta vya Kampuni ya Puma Energy Tanzania Ltd, wakati wa utoaji tuzo hizo, Dar es Salaam. Kutoka kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hiyo, Dominic Dhanah na Mwenyekiti wa Bodi ya Kampuni ya Puma Energy Tanzania Ltd.
WASHINDI wa tuzo mbalimbali wakiwa katika picha ya pamoja na Waziri wa Nishati, Dk. Medard Kalemani na viongozi wa Kampuni ya Puma Energy Tanzania, wakati wa tuzo za waendesha vituo vya mafuta vya Kampuni ya Puma Energy Tanzania Ltd.
WASHIRIKI wa tuzo za waendesha vituo vya mafuta vya Kampuni ya Puma Energy Tanzania Ltd, wakifuatilia utoaji wa tuzo hizo, Dar es Salaam.


from MICHUZI BLOG https://ift.tt/2Se7hxb
via
logoblog

Thanks for reading KAMPUNI YA MAFUTA YA PUMA TANZANIA YATOA TUZO, ZAWADI KWA WAENDESHA VITUO VYA MAFUTA NCHINI

Previous
« Prev Post