KABENDERA AANZA KUONA NURU DHIDI YA KESI YAKE.

  Masama Blog      
UPANDE wa mashitaka katika kesi ya uhujumu uchumi inayomkabili  mwandishi wa Habari za uchunguzi Erick Kabendera umeiomba Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuwapa ruhusa ya kuzungumza binafsi na mshtakiwa leo ili kukamilisha makubaliano ya kukiri kosa lake ambayo yameishafikia mwisho.

Jopo la Mawakili watatu wa Serikali ukiongozwa na wakili wa Serikali Mkuu Faraja Nchimbi  wamewasilisha maombi hilo  mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi Janet Mtega wakati kesi hiyo ilipofika mahakamabi hapo kwa ajili ya kutajwa na kujua hatma ya makubaliano yao na DPP.

"Mazungumzo ya kukiri makosa kati ya Kabendera ma Mkurugenzi wa Mashtaka Nchini (DPP) yapo kwenye hatua za mwisho hivyo tunaomba mazungumzo binafsi na mshtakiwa ili yeye mwenyewe aweze kukiri mashtaka yake tuendelee na taratibu za kisheria kwani kwa kipindi kirefu cha mazungumzo tulikuwa tukizungumza na mawakili wa upande wa utetezi bila ya kuwepo kwa mshtakiwa mwenyewe", amedai Nchimbi.

Amedai, mazungumzo hayo yapo kisheria kifungo cha 3 na kifungu cha 194 A na H cha sheria ya makosa ya jinsi cha mwaka 1985 sura ya 20(plea Bargaining) ambapo mtuhumiwa anapewa nafasi ya kukiri kosa na kuomba msamaha na baadae kuachiwa huru.

Wakili wa utetezi, Gebra Kambore amesema hana pingamizi juu maombi hayo ya upande wa mashtaka na kesi hiyo imeahirishwa hadi Jumatatu Februari  17, mwaka huu.

Katika kesi hiyo, Kabendera anakabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi yenye mashtaka matatu ya utakatishaji wa Sh milioni 173.2, kujihusisha na mtandao wa kihalifu kwa kutoa msaada kwa genge la uhalifu kwa nia ya kujipatia faida na kukwepa kodi.

Inadaiwa kuwa kati ya Januari 2015 na Julai Mwaka jana jijini Dar es Salaam bila ya sababu, alikwepa kodi ya Sh 173,247,047.02 ambayo ilitakiwa ilipwe Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).

Pia inadaiwa Kabendera alitakatisha Sh 173,247047.02 huku akijua fedha hizo ni mazalia ya kosa la kujihusisha na genge la uhalifu na ukwepaji kodi.

Katika makosa hayo baadhi anadaiwa kutenda kwa ushirikiano na watu ambao hawajakamatwa


from MICHUZI BLOG https://ift.tt/2tNxZ7T
via
logoblog

Thanks for reading KABENDERA AANZA KUONA NURU DHIDI YA KESI YAKE.

Previous
« Prev Post