JPM KUZINDUA WILAYA MPYA YA KIGAMBONI KESHO

  Masama Blog      
Na Leandra Gabriel, Michuzi TV
RAIS Dkt. John Magufuli kesho Februari 11 atazindua rasmi Wilaya mpya ya Kigamboni ambayo ni zao la Wilaya ya Temeke na hiyo ni baada ya makao makuu ya Wilaya hiyo kukamilika.

Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam, Mkuu wa Mkoa Paul Makonda amesema kuwa;

"Kesho Rais Magufuli atazindua rasmi makao ya Wilaya ya Kigamboni na shughuli itafanyika katika viwanja vya mkuu wa Wilaya ya Kigamboni kuanzia saa mbili asubuhi" amesema.

Aidha amesema kuwa Wilaya hiyo imekamilika kwa kiasi kikubwa na kuwa na ofisi za Mkuu wa Wilaya, utawala, Manispaa pamoja na huduma muhimu ikiwemo afya na elimu.

Makonda amesema kuwa Rais Magufuli amefanikisha ujenzi wa hospitali ya Wilaya ya Kigamboni ujenzi uliogharimu shilingi bilioni 1.5 na hiyo ni pamoja na ujenzi na uimarishaji wa sekta za zahanati, elimu, umeme, maji pamoja na ujenzi wa barabara mpya (kilomita 75) kwa gharama ya shilingi bilioni 90.

Vilevile RC Makonda amewataka wakazi wa Dar es Salaam kujitokeza kwa wingi katika uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura mchakato utakaoanza Februari 14 hadi 20 mwaka huu ambapo amewataka wananchi kutumia haki yao ya kikatiba kupitia mchakato huo.


from MICHUZI BLOG https://ift.tt/2vgGhpg
via
logoblog

Thanks for reading JPM KUZINDUA WILAYA MPYA YA KIGAMBONI KESHO

Previous
« Prev Post