Idara ya Uhamiaji Yashiriki Kikamilifu Wiki ya Sheria Tanzania Mkoani Kilimanjaro

  Masama Blog      
Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Dkt. Anna Mghwira akisikiliza maelezo toka kwa Mrakibu msaidizi wa Uhamiaji, Sale Sule alipotembelea banda la Uhamiaji katika maonesho ya wiki ya sharia yanayoendelea kufanyika katika Viwanja vya Mahakama katika manispaa ya Moshi.
Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Dkt. Anna Mghwira  akipata maelezo ya Pasipoti mpya za Kielektroniki toka kwa Mrakibu Msaidizi wa Uhamiaji Sale Sule wakati alipotembelea banda la uhamiaji kwenye  ufunguzi wa wiki ya sharia mkoani Kilimanjaro.
Mrakibu wa Uhamiaji Grace Malagila akishiriki kikamilifu mazoezi ya viungo ya pamoja yaliyoongozwa na Mhe. Dkt Anna Mghwira  (hayupo pichani) kabla ya ufunguzi rasmi wa wiki ya sharia. Wadau mbalimbali walishiriki katika mazoezi hayo, vikiwemo vyomba vya ulinzi na usalama.
Mkaguzi msaidizi wa Uhamiaji Dorothy Ngai akifafanunua jambo kwa moja ya wadau waliotembelea banda la Uhamiaji katika maonesho ya wiki ya sharia. Pembeni ni Koplo Vedastus Ng’aire.
Mkaguzi Msaidizi wa Uhamiaji Octavia Makwawa akifafanunua jambo kwa moja ya wadau waliotembelea banda la Uhamiaji katika maonesho ya wiki ya sharia. Pembeni ni  Konstebo Innocent Mshana.

Wadau mbalimbali wakishiriki matembezi maaulu yaliyoandaliwa na Idara ya Mahakama katika ufunguzi wa maadhimisho ya waiki ya sharia Mkoani Kilimanjaro. Idara ya Uhamiaji kwa Kushirikiana na Chuo cha Uhamiaji – TRITA, walishiriki kikamilifu katika matembezi hayo.

……………………………………………………

KAULIMBIU: 

“uwekezaji na biashara jukumu la mahakamana wadau kuweka mazingira wezeshi ya uwekezaji”

Na Afisa Uhusiano & Itifaki- TRITA

Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Mhe. Dkt. Anna Mghwira ameitaka Mahakama kutoa haki kwa wote bila kujali uwezo wa kipato kwa wanaokuja kupata huduma za kimahakama katika ofisi husika. Mhe. Mghwira amesema hayo jana tarehe 31 Januari 2020 wakati wa ufunguzi   rasmi wa wiki ya Sheria Mkoa wa Kilimanjaro.

Aidha, katika maadhimisho hayo yaliyotanguliwa kwa maandamano yaliyoshirikisha taasisi mbalimbali vikiwemo vyombo vya Ulinzi na Usalama ikiwemo Idara ya Uhamiaji yalipambwa kwa matukio mbali mbali kama vile mozoezi ya pamoja, matembezi ya umbali wa kilometa tatu pamoja na ufunguzi rasmi wa mabanda ya maenesho.

Mhe. Mkuu wa Mkoa alipata nafasi ya kutembelea  banda la Uhamiaji, ambapo alipewa elimu kuhusiana na utolewaji wa pasipoti mpya za kielektoniki na mikakati mbalimbali  aliyowekwa na Idara ya Uhamiaji katika kupambana na wimbi la wahamiaji haramu.

Mhe. Mghwira alifurahishwa na maelezo yaliyotolewa na Mrakibu Msaidizi wa Uhamiaji Sale Sule ambaye sharia, kanuni na miongozo huku akisisitiza udhibiti wa mipaka na wahamiaji haramu ambao wamekuwa wakiingia kwa wingi pia ni Mwanasheria wa Uhamiaji Mkoa wa Kilimanjaro.

Kabla ya kumaliza ziara yake katika banda ya Uhamiaji, Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Dkt. Anna Mghwira aliitaka Ofisi ya Uhamiaji Mkoa wa Kilimanjaro kufanya kazi kwa kuzingatia kupitia njia za panya  hapa nchini wakitokea nchi jirani.


from MICHUZI BLOG https://ift.tt/2OiKv68
via
logoblog

Thanks for reading Idara ya Uhamiaji Yashiriki Kikamilifu Wiki ya Sheria Tanzania Mkoani Kilimanjaro

Previous
« Prev Post