Hakuna viza kwa afanyakazi wasiokuwa na ujuzi Uingereza

  Masama Blog      
Wafanyakazi wasiokuwa na ujuzi hawatapata viza chini ya mpango mpya wa uhamiaji wa serikali baada ya Uingereza kujiondoa katika Muungano wa Ulaya.

Serikali inahamasiha waajiri kuacha kutegemea wafanyakazi wa kulipwa mshahara wa chini kutoka Ulaya na kuwekeza zaidi katika kudumisha wafanyakazi na kuendelezea teknolojia.

Wizara ya mambo ya ndani imesema Ulaya na raia wa nchi ambazo sio wanachama wa Muungano huo watakuwa wanachukuliwa walio katika daraja moja baada ya usafiri huru kati ya Uingereza na Muungano wa Ulaya kufikia ukomo wake Desemba 31.

Makampuni yanasema sheria kali kama hizo zitafanya iwe vigumu kuvutia wafanyakazi.

Lakini waziri wa mambo ya ndani Priti Patel amesema utekelezaji wa mfumo mpya kutamaanisha watu wenye weledi tu ndio watakaoingia Uingereza.
 


from MICHUZI BLOG https://ift.tt/2VeNiSv
via
logoblog

Thanks for reading Hakuna viza kwa afanyakazi wasiokuwa na ujuzi Uingereza

Previous
« Prev Post