GCLA YAWAPIGA MSASA WASIMAMIZI WA KEMIKALI KANDA YA MASHARIKI

  Masama Blog      
WASIMAMIZI wa Kemikali zaidi ya 30 wa Kanda ya Mashariki wamepatiwa mafunzo maalumu ya siku mbili juu ya usimamizi salama wa kemikali kwa wasimamizi wa kemikali katika viwanda, makampuni na taasisi za Serikali.

 Mafunzo hayo yaliandaliwa na Kanda ya Mashariki ya siku mbili, yalifungwa rasmi na Kaimu Mkemia Mkuu wa Serikali, Sabanitho Mtega, katika ukumbi wa TACAIDS Dae es SalĂ am.

Kaimu mkemia mkuu wa Serikali, Mtega amewataka kutumia elimu waliyoipata katika kusimamia kwa umakini matumizi ya kemikali kwa lengo la kulinda afya za binadamu na mazingira na kawapatia elimu hiyo wafanyakazi wanaowasimamia.

Mtega aliongeza kuwa, washiriki hao wataweza kuepusha majanga yanayosababishwa na kemikali kutokana na mafunzo waliyopata

Awali Wasimamizi hao wa kemikali waliishukuru Kanda ya Mashariki kwa kuwapatia mafunzo ya Usimamizi salama wa kemikali kwenye maeneo yao ya kazi.

Wamebainisha kuwa, mafunzo hayo yatawasaidia katika kuboresha utekelezaji wa majukumu  yao ya kila siku ambayo yanahitaji matumizi ya kemikali.
 Mwezeshaji wa mafunzo ya matumizi salama ya Kemikali, Hadija Mwema (kulia) akiwasilisha mada kuhusu kadi ya usalama wa kemikali kwa wasimamizi wa kemikali kutoka kwenye makampuni, mashirika na viwanda vinavyojihusisha na kemikali.
 Kaimu Mkemia Mkuu wa Serikali, Sabanitho Mtega ( kulia) akimkabidhi mshiriki wa mafunzo cheti cha kuhitimu mafunzo ya usimamizi salama wa kemikali yaliyohiyimishwa leo Dar es Salaam.
 Kaimu Mkemia Mkuu wa Serikali, Sabanitho Mtega (wa pili kulia, waliokaa) akiwa pamoja na baadhi ya wawezeshaji na washiriki wa mafunzo ya usimamizi salama wa kemikali yaliyoandaliwa na Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali, Kanda ya Mashariki, Dar es Salaam.from MICHUZI BLOG https://ift.tt/2HG50Go
via
logoblog

Thanks for reading GCLA YAWAPIGA MSASA WASIMAMIZI WA KEMIKALI KANDA YA MASHARIKI

Previous
« Prev Post