DC TANDAHIMBA AWAOMBA WANANCHI KUJITOKEZA KWA WINGI WIKI YA SHERIA KUPATA HUDUMA ZA KISHERIA

  Masama Blog      
Mkuu wa Wilaya ya Tandahimba Sebastian Waryuba amewaomba wananchi wajitokeze ili waweze kupata huduma ya kisheria katika wiki hii ya Sheria.

Waryuba alisema kuwa wananchi wanaonekana elimu ya wiki ya Sheria hawana ya kutosha  ndiyo maana hawajitokezi kwa wingi kupata huduma hii

Akizungumza katika uzinduzi wa wiki ya sheria katika viwanja vya mahakama ya Wilaya, Waryuba alieleza kuwa kauli mbiu ya mwaka huu uwekezaji na biashara ni  wajibu wa mahakama  na wadau kuweka mazingira wezeshi ya uwekezaji inaendana na maendeleo ya sekta ya viwanda nchini.

"Wananchi wanahitaji elimu kuhusu wiki hii ya Sheria ili waweze kupata huduma za kisheria bure ,lakini inaoneha wengi wao bado uelewa ni mdogo kuhusu wiki hii,alisema Waryuba.

Naye Hakimu Mkazi Mfawidhi Joseph Waruku alieleza kuwa moja ya maboresho ya nguzo ya mahakama ni kubadilisha mtazamo wa wananchi kuhusu taswira ya mahakama ili kuongeza Imani ya wananchi na wadau kwa ujumla

Waruku alieleza kuwa lengo la wiki ya  Sheria ni kutoa elimu kwa wananchi 

"Mahakama ni chombo ambacho kinatoa haki kwa kufuata kanuni ,"alisema Waruku.
  Baadhi ya wanafunzi ambao walijitokeza kuunga mkono maandamano  ya wiki ya sheria.
DC Waryuba akizungumza jambo wakati wa uzinduzi wa wiki ya Sheria
 Hakimu Mkazi Mfawidhi    wa Mahakama ya Wilaya ya Tandahimba Joseph Waruku akieleza umuhimu wa wiki ya sheria
Maadhimisho ya wiki ya sheria Wilayani Tandahimba yaliambatana na maandamano  ambao yalipokewa na Dc Waryuba


from MICHUZI BLOG https://ift.tt/2GMByxW
via
logoblog

Thanks for reading DC TANDAHIMBA AWAOMBA WANANCHI KUJITOKEZA KWA WINGI WIKI YA SHERIA KUPATA HUDUMA ZA KISHERIA

Previous
« Prev Post