CRDB YADHAMIRIA KUINUA HALI ZA KIUCHUMI KWA WANANCHI WA MIJINI NA VIJIJINI KWA KUIBUA MIRADI MBALI MBALI

  Masama Blog      
Uongozi wa Benki ya CRDB Nchini umeazimia kuunga mkono Utekelezaji wa miradi mbali mbali ya Maendeleo inayowagusa moja kwa Moja Wananchi kwa kushirikiana na Serikali katika kuona ustawi wa Jamii Mjini na Vijijini unaimarika kila siku.

Akizungumza na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi Vuga Mjini Zanzibar Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo ya CRDB Bwana Abdulmajid Mussa Nsekela  amesema Benki hiyo iliyopata Tuzo ya Mfuko wa Kimataifa wa Mazingira itadhihirisha Utekelezaji wa Fasafa yake  kwa kuendeleza dhamira ya kutoa huduma bora kwa Umma kwa kutumia mfumo wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano {|TEHAMA}.  
                                              
Akitoa shukrani zake Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi ameupongeza Uongozi wa Benki hiyo ya CRDB kwa sera zake zilizojikita kusaidia Wananchi hasa Sekta ya Ujasiriamali.

Balozi Seif amesema inapendeza kuona Benki hiyo bado haijawahi kutetereka kama zilivyowahi kutokea baadhi ya Taasisi nyengine za Kifedha Nchini kutokana na kuongezeka kwa idadi ya Wanachama kila Mwaka.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar ameeleza kwamba CRDB ni Benki inayowalenga moja kwa moja Wananchi walio wengi hasa wale wa Vijijini wanaojishughulisha zaidi na Sekta ya Kilimo ambayo ndio tegemezi kuu la Pato la Taifa.


Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akiusikiliza Uongozi wa Benki ya CRDB Nchini,ulioongozwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo ya CRDB Bwana Abdulmajid Mussa Nsekela,alipokutana nao Ofisni kwake Vuga Mjini Zanzibar

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akizungumza na
Uongozi wa Benki ya CRDB Nchini,ukiongozwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo ya CRDB Bwana Abdulmajid Mussa Nsekela,Vuga Mjini Zanzibar


from MICHUZI BLOG https://ift.tt/39xcwz2
via
logoblog

Thanks for reading CRDB YADHAMIRIA KUINUA HALI ZA KIUCHUMI KWA WANANCHI WA MIJINI NA VIJIJINI KWA KUIBUA MIRADI MBALI MBALI

Previous
« Prev Post