China yaripoti kuongezeka kwa idadi ya maambukizi ya virusi vya Corona,vyafikia 908.

  Masama Blog      
China imeripoti kuongezeka kwa idadi ya visa vya maambukizi ya virusi vya Corona na huenda hali hiyo ikadidimiza matumaini kwamba hatua za udhibiti wa virusi hivyo zinafanya kazi.

Idadi ya waliofariki kutokana na virusi vya corona nchini China bara imefikia watu 908, baada ya vifo vipya 97 kuripotiwa katika muda wa saa 24 hapo jana usiku. Wakati huo huo nchi hiyo imesajiri visa vipya 3,062 vya ugonjwa huo.

Hiyo ni nyongeza ya asilimia 15 kutoka siku ya Jumamosi ambayo imegeuza mwelekeo ambapo kila siku maambukizi mapya yamekuwa yakipungua. Hapo jana, msemaji wa serikali alisema kuwa idadi ya visa vya maambukizi iliyopungua ilionyesha kuwa mikakati ya kuzuia kuenea kwa virusi hivyo imefanikiwa.

Nahodha wa meli ya anasa iliyowekwa chini ya karantini mjini Yokohama karibu na mji mkuu wa Japan, Tokyo, amesema kuwa visa 66 vipya vya maambukizi ya homa ya corona viligunduliwa katika meli hiyo. Hili ni ongezeko katika visa 70 vilivyokuwa vimeripotiwa awali.Waziri wa afya wa Japan Katsunobu Kato, amesema kuwa serikali ya Japan inafikiria kuwafanyia uchunguzi abiria wote 3,771 na wafanyikazi wa meli hiyo ya Diamond Princess ambapo watu hao watalazimika kusalia katika meli hiyo hadi majibu ya uchunguzi huo yatakapotolewa.

Maafisa wa afya wanajitahidi kupeleka dawa zinazohitajiwa na abiria zaidi ya 600. Kato amesema kuwa wanajitahidi kadri ya uwezo wao kuhakikisha kuwa kila mmoja anasalia kuwa na afya njema. Zaidi ya visa 360 vimethibitishwa nje ya China bara ikiwa ni pamoja na vifo viwili katika jimbo la Hong Kong ambalo pia limethibitisha visa 36, pamoja na Ufilipino.

Wakati huo huo, serikali ya Uingereza hii leo imeonya kuwa mripuko huo wa virusi vya Corona ni hatari kwa umma na kutangaza mikakati mipya ya kuwalinda raia wake. Taarifa kutoka kwa wizara ya afya imesema kuwa kuenea kwa virusi hivyo kunahusisha tishio kubwa kwa afya ya umma.

from MICHUZI BLOG https://ift.tt/2OKv9b0
via
logoblog

Thanks for reading China yaripoti kuongezeka kwa idadi ya maambukizi ya virusi vya Corona,vyafikia 908.

Previous
« Prev Post