DOWNLOAD APP YETU HAPA

Chama kikuu cha upinzani cha CNL kimemuidhinisha Agathon Rwasa kuwa mgombea wake wa kiti cha urais

  Masama Blog      
Chama kikuu cha upinzani nchini Burundi kimemuidhinisha Agathon Rwasa kuwa mgombea wake katika uchaguzi wa rais wa Mei 20 mwaka huu.

Wajumbe wa chama cha National Congres for Liberty jana walimuidhinisha Rwasa aliye na umri wa miaka 56 kama mgombea wao katika uchaguzi wa Rais wa mwezi Mei.

Agathon Rwasa atachuana katika uchaguzi huo na Jenerali wa jeshi Evariste Ndayishimiye ambaye ni muitifaki wa Nkurunzia. Mwezi uliopita chama tawala Burundi CNDD-FDD kilimchagua jenerali huyo wa jeshi kupeperusha bendera ya chama hicho.

Jana Jumapili Agathon Rwasa alisema kuwa inashangaza kusikia sasa kwamba kuna watu wanaofikiria kuchakachua uchaguzi. Aliyasema hayo mbele ya wajumbe wa chama chake baada ya kutangazwa uteuzi wake. Rwasa alisema wananchi wa Burundi hawataruhusu kujiri wizi wa kura.
 
KUSOMA HABARI ZAIDNI BOFYA HAPA 


from MICHUZI BLOG https://ift.tt/322HyfO
via
logoblog

Thanks for reading Chama kikuu cha upinzani cha CNL kimemuidhinisha Agathon Rwasa kuwa mgombea wake wa kiti cha urais

Previous
« Prev Post