CHADEMA YATIKISIKA KILOMBERO,VIONGOZI WAKE WAJIVUA UANACHAMA NA KUHAMIA CCM

  Masama Blog      
VIONGOZI wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema wilaya ya Kilombero wamejivua uanachama wa Chadema hicho  na kujiunga na Chama cha Mapinduzi CCM.

Waliojivua uanachama wa Chadema ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji wa Ifakara CHADEMA, Mashaka Mbilinyi, Diwani kata ya Mbasa ,Chiza  Shungu, Mwenyekiti wa kamati huduma za Jamii Ifakara, Digna Nyangile, Diwani Viti Maaalum Ifakara, Antony Mwampunga Kamanda wa Red Briged wilaya Kilombero, Clarens  Manyota na Baraka Masala.

Wanachama hao wapya wamepokewa na  Katibu Mkuu wa CCM Dk Bashiru Ali Kakurwa  na kukabidhiwa kadi za uanachama wakati wa mkutano wake wilayani humo, ambapo amepata nafasi ya kuongea na viongozi na wanachama wa chama hicho.

Dkt.Bashiru yupo mkoani Morogoro kwa ziara ya siku tatu kuona miradi mbalimbali na utekelezaji wa ilani ya Chama cha CCM.

Kwa upande wake Katibu wa Chama hicho Mkoa wa Morogoro,Shaka Hamdu Shaka amesema wanachama hao waliojiunga na Chama cha CCM ni kutokana na kuona juhudi za chama katika kufanya kazi na  maendeleo katika  kutekeleza ilani za Chama cha Mapinduzi.

Amesema kutokana na kazi kubwa inayofanya na Chama hicho kwa sasa katika kuwatumikia wananchi wapinzani wengi wameamua kurudi CCM .

Wakati huo huo Mbunge wa Viti Maalum wa Jimbo la Kilombero,Mama Gertrude Lwakatale amekabidhi Pikipiki 22 kwaajili ya Chama cha CCM ambazo zitatumika kipindi cha kampeni zitakapoanza .

Amesema tayari alitoa baskeli 300 kwa Chama hicho ikiwa na nia ya kukisaidia katika kuleta maendeleo ya chama ndani ya jimbo lake.
Katibu wa Chama cha Mapinduzi CCM Bushiru Ali akimpa mkono  Mbunge wa viti Maalum wa wilaya  ya kilombero Dkt.Getrude Lwakatare  wakati wa ziara yake ya kutembelea miradi mbalimbali ya Chama hicho mkoani Morogoro wengine ni viongozi wa Mkoa wa Chama hicho.
Katibu wa Chama cha Mapinduzi CCM ,Dkt.Bashiru Ali akiwa amepanda pikipiki moja wapo iliyotolewa na   Mbunge wa viti Maalum wa wilaya  ya kilombero Dkt.Getrude Lwakatare aliyeko kushoto kwa ajili ya kusaidia kazi za Chama kipindi cha Uchaguzi.
Mwenyekiti wa halmashauri wa mji wa ifakara ,Mashaka Mbilinyi akikabidhiwa kadi  ya uanachama na Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM ,Dkt.Bashiru Ali  wilayani Kilombero.


from MICHUZI BLOG https://ift.tt/2HkdTFs
via
logoblog

Thanks for reading CHADEMA YATIKISIKA KILOMBERO,VIONGOZI WAKE WAJIVUA UANACHAMA NA KUHAMIA CCM

Previous
« Prev Post