CCM MIHAMBWE YARIDHISHWA NA UTEKELEZAJI ILANI YA UCHAGUZI

  Masama Blog      

Na Mwandishi wetu Mihambwe

Kamati za siasa za kata tano zinazounda Tarafa ya Mihambwe zimeridhishwa ma utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya mwaka 2015 - 2020 ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) uliofanywa ndani ya Tarafa hiyo katika miradi mbalimbali ya elimu, afya, kilimo, umeme, ardhi, miundombinu na maendeleo ya jamii.

Hayo yamebainishwa na Katibu wa Makatibu CCM wilaya Tandahimba ambaye pia ni Katibu kata ya Kitama, Ndugu Ahmed Hassan Mkobo wakati wa maadhimisho ya sherehe za miaka 43 ya kuzaliwa CCM ambapo walitembelea maeneo mbalimbali kukagua utekelezaji wa miradi ya kimaendeleo iliyotekelezwa ndani ya Tarafa hiyo katika kipindi cha Serikali ya awamu ya tano chini ya Mhe. Rais Dkt. John Magufuli,  amesema CCM imeridhishwa na utekelezaji wa ilani ya uchaguzi iliyofanyika.

"Kote tulipopita tumejionea uadilifu, uzalendo na uchapa kazi wa viongozi wa Serikali uliopelekea kufanya vyema utekelezaji wa ilani ya uchaguzi. CCM tumeridhishwa na maendeleo tuliyoyaona. Nawapongeza sana kwa kazi kubwa na nzuri ya utekelezaji wa miradi ya kimaendeleo." Alisema Ndugu Ahmed Hassan Mkobo.

Akizungumza mara baada ya kumalizika ziara hiyo, Afisa Tarafa Mihambwe Emmanuel Shilatu amewashukuru viongozi wa CCM kutambua juhudi kubwa ya utekelezaji wa ilani ya uchaguzi waliyoiona. Shilatu amewahakikishia ushirikiano viongozi hao CCM katika kuhakikisha yote yaliyohaidiwa na Mhe. Rais Magufuli  yanatekelezwa ndani ya Tarafa ya Mihambwe.

Kamati za siasa za kata za Kitama, Mihambwe, Miuta, Michenjele na Mkoreha zilifanya ziara kukagua utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ulivyo ndani ya Tarafa ya Mihambwe.
 


from MICHUZI BLOG https://ift.tt/2ODBCEB
via
logoblog

Thanks for reading CCM MIHAMBWE YARIDHISHWA NA UTEKELEZAJI ILANI YA UCHAGUZI

Previous
« Prev Post