CBA Tanzania na Vodacom Wakabidhi mil 10 kwa Mshindi wa Promosheni ya TUNZA UTUNZWE NA M-PAWA

  Masama Blog      

Mwakilishi wa Benki ya CBA, Bi. Gloria Njiu (kushoto) akimkabidhi mfano wa hundi yenye thamani ya shilingi milioni 10/- kwa mshindi wa shindano la promosheni ya TUNZA UTUNZWE NA M-PAWA, Joseph Mkombozi kutoka Kijiji cha Makole, Muheza mkoani Tanga, hafla ya makabidhiano ilifanyika viwanja vya Zakhem Mbagala jijini Dar es salaam jana. Katikati ni Meneja Masoko CBA, Solomon Kawiche.
Mwakilishi wa Benki ya CBA, Bi. Gloria Njiu (kushoto) akimkabidhi mfano wa hundi yenye thamani ya shilingi milioni 10/- kwa mshindi wa shindano la promosheni ya TUNZA UTUNZWE NA M-PAWA, Joseph Mkombozi kutoka Kijiji cha Makole, Muheza mkoani Tanga, hafla ya makabidhiano ilifanyika viwanja vya Zakhem Mbagala jijini Dar es salaam jana.
Benki ya CBA Tanzania kwa kushirikiana na Vodacom leo wamekabidhi kitita cha sh. Milioni 10 kwa Joseph Mkombozi (23), kutoka Kijiji cha Makole, Muheza mkoani Tanga, baada ya kuibuka mshindi katika Promosheni ya TUNZA, UTUNZWE NA M-PAWA.

Mpawa ni huduma inayotolewa kwa ushirikiano wa Vodacom na CBA bank, Huduma inayomwezesha mtumiaji wa mtandao wa Vodacom kukopa fedha na kuhifadhi hela kupitia simu yake ya mkononi, ni bank kwenye kiganja cha mtumiaji.

Akizungumza baada ya kukabidhiwa hundi yake ya shilingi milioni kumi, Mkombozi aliishukuru benki ya CBA kwa ubunifu wake wenye lengo la kuinua maisha ya watanzania. “Niwashukuru CBA kwa wazo hili ambalo kwa kiasi kikubwa linamfaidisha mtanzania wa aina yoyote ile atakayekuwa ameshiriki,” alisema.

Mwakilishi wa Benki ya CBA, Bi. Gloria Njiu, alisema kuwa, tangu kuanza kwa promosheni hii Oktoba mwaka jana, kumekuwa na washindi mbalimbali wakiwamo waliojishindia bodaboda. “Wakati tunahitimisha promosheni hii kwa kumzawadia mshindi wa milioni 10, ifahamike kuwa tumekuwa na washindi wengine zaidi ya 300 ambao walijishindia bodaboda na mara mbili ya amana zao walizohifadhi kwenye M-Pawa” alisema Gloria

Kwa mujibu wa Glory washindi waliojishindia boda boda ni pamoja na Christina Toto, (Manyara), Johnson Mollel (Arusha), Fravianus Frugence (Bukoba Mjini), Letisia Yohana (Dar es Salaam), Herman Mwakapeje (Mbeya) na Egiduis Buberwa (Tabora).

Wengine ni Grace Mollel (Arusha), Musa Kuyava (Iringa), Joseph Renatus (Shinyanga), Sadiki Rashidi (Dodoma), Emmanuel Tesha (Iringa), Grace Ginesasi (Mbeya), John Joseph (Moshi Mjini), Daudi Daudi ( Bunju), Mwashabani Kiegebu (Zanzibar), Fidelis Mfuse (Njombe), Angelina Mkota (Dodoma) na Aswile Mapanga kutoka Mbeya Mjini.

Tangu kuanzishwa kwa huduma ya M-Pawa, watumiaji wake wameongezeka kwa kasi hadi kufikia milioni 9 nchini kote. Wateja wa huduma hii ni wafanya biashara wadogo wadogo, wakulima na hasa maeneo ya vijijini ambapo huduma za benki ni za kiwango kidogo kwasababu ya ukosefu wa taasisi za benki na upungufu wa mahitaji ya kifedha.

M-Pawa imekuwa ikihudumia mamilioni ya watanzania katika kila kona ya nchi. Huduma hii imerahisisha huduma za kibenki za kuweka na kuchukua mkopo bila kwenda kwenye tawi la kibenki au kutumia makaratasi. Bali kwa simu yako ya mkononi tu, unaweza weka akiba na kuomba mkopo

Promosheni hii ya TUNZA, UTUNZWE NA M-PAWA iliyoanza Novemba mwaka jana na kufikia kilele chake wiki iliyopita, ililenga kuwazadia wateja wote wa huduma ya M-Pawa.

Ili kushiriki na kushinda, mteja wa M-PAWA alitakiwa kuweka akiba mara nyingi iwezekanavyo, kukopa na kurudisha mapema mkopo wake na hapo alikuwa ameingia kwenye droo na kujiwekea nafasi ya kushinda.


from MICHUZI BLOG https://ift.tt/3bnDWsW
via
logoblog

Thanks for reading CBA Tanzania na Vodacom Wakabidhi mil 10 kwa Mshindi wa Promosheni ya TUNZA UTUNZWE NA M-PAWA

Previous
« Prev Post