BASHUNGWA: TUUNGE MKONO BIDHAA ZA NDANI ‘MADE IN TANZANIA’

  Masama Blog      Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe.Innocent Bashungwa akizungumzana Waandishi wa Habari (hawapo pichani) kuhuhu bidhaa za kiwanda cha vifaa vya umeme cha Africab Jijini Dar es Salaam kinachozalisha vifaa mbalimbali ikiwemotransfoma, katika mwendelezo wa Ziara ya kutembelea viwanda Jijini Dar esSalaam.
Baadhi ya Vifaa vya Umeme vinavyozalishwa na kiwanda cha Africabkilichopo Jijini Dar es salaam, kiwanda hicho kinatengeneza vifaa mbalimbalizikiwemo transfoma na nyaya za umeme.
Moja ya Transfoma inayotengenezwa na Kiwanda cha Africab kilichopoJijini Dar es salaam, ambapo Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe.InnocentBashungwa alitembelea na kutoa rai kwa watanzania kutumia bidhaa zitokanazo naviwanda vya ndani.
Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe.Innocent Bashungwa, Katibu Mkuu waWizara hiyo, Prof. Riziki Shemdoe na wamiliki wa kiwanda kuzalisha vifaa vyaUmeme cha Tropical kilichopo Dar es Salaam, Bw.Charles Mlawa na Aloyce Ngowibaada ya kutembelea kiwandani hapo leo Februari 19, 2020 katika Mwendelezo waziara ya kutembelea viwanda Jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe.Innocent Bashungwa, Katibu Mkuu waWizara hiyo, Prof. Riziki Shemdoe wakisikiliza maelezo kutoka kwa Mkurugenzi waKiwanda cha Tropical kilichopo Dar es Salaam, Bw. Aloyce Ngowi walipotembeleakiwandani hapo leo Februari 19, 2020 katika Mwendelezo wa ziara ya kutembeleaviwanda Jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya mashine za kutengeneza vifaa vya umeme zilizopokatika kiwanda cha Tropical kilichopo Jijini Dar es Salaam kama zinavyoonekanakwenye picha kiwanda hicho kinatengeneza vifaa mbalimbali zikiwemo transfoma,nyaya za umeme na soketi za umeme.
Mashine ya kusokota nyaza umeme iliyopo katika kiwanda chaTropical kilichopo Jijini Dar es Salaam kama inavyoonekana kwenye picha, kiwandahicho kinatengeneza vifaa mbalimbali zikiwemo transfoma, nyaya za umeme nasoketi za umeme.
Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe.Innocent Bashungwa, Katibu Mkuu waWizara hiyo, Prof. Riziki Shemdoe wakisikiliza maelezo kutoka kwa Mkurugenzi waKiwanda cha Tropical kilichopo Dar es Salaam, Bw. Aloyce Ngowi jinsi yakutengeneza transfoma walipotembelea kiwandani hapo leo Februari 19, 2020katika Mwendelezo wa ziara ya kutembelea viwanda Jijini Dar es Salaam.
Wafanyakazi kutoka kiwanda cha kutengeneza vifaa vyaumeme cha Tropical kilichopo Jijini Dar es Salaam, wakitenegeneza Transfomabaada ya Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe.Innocent Bashungwa kutembeleakiwanda hicho katika mwendelezo wa ziara ya kutembelea viwanda Jijini Dar esSalaam.
Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe.Innocent Bashungwa, akisalimiana naMfanyakazi wa kiwanda cha Tropical katika kitengo cha kutengeneza soketi katikakiwanda hicho kilichopo Jijini Dar es Salaam.
Transfoma na Vifaa vingine vya umeme kutoka kiwanda cha Tropicalambapo Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe.Innocent Bashungwa alitembeleakatika mwendelezo wa ziara ya kutembelea viwanda Jijini Dar es Salaam kamavinavyoonekana kwenye picha.Picha na Idara ya Habari-MAELEZO.
……………………………………………………………………………………………………
Na. Eric Msuya – MAELEZO.
.
 
Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Innocent Bashungwa amewatakawadau wa Viwanda na Biashara kuendelea kuunga mkono Serikali yaawamu ya tano kwa kuendelea kutoa ajira katika viwanda vidogo navikubwa ili kupunguza adha ya ukosefu wa ajira kwa vijana Nchini.
Ameyasema hayo leo Jumatano katika mwendelezo wa ziara yake yakutembelea Viwanda vilivyopo Jijini Dar es salaam na kutoa rai kwakwa watanzania kutumia bidhaa zinazotokana na viwanda vya ndani ilikuongeza ajira kwa vijana

“Hongereni kwa kumuunga mkono Rais wetu Magufuli kwa kuwapa ajirawatanzania 150, ambao ni wahitimu wa vyuo mbalimbali hapa nchini,lakini hata wale walikuwa nyumbani wamekaa bila kazi” alisema Mhe.Bashungwa
 Katika Ziara hiyo Mhe. Bashungwa amewapongeza Bwana CharlesMlawa na Aloyce Ngowi ambao ni wamiliki wazawa wa kiwanda chaTropical kilichopo Jijini Dar es Salaam kinachozalisha Vifaa vya Umeme(Soketi na Transfoma) hapa Nchini kwa lengo la kuunga mkono Serikalikufikia Uchumi wa kati wenye viwanda.
 “Nyie ni wazalendo, ni mfano tosha kwa wawekezaji wazawa kwakufahamu umuhimu wa Serikali kufikia uchumi wa kati, transfoma nanyanya za kupitishia umeme zote zenye ubora sasa zinatengenezwaTanzania tena mwenge, Dar es Salaam, na sio tena kuagiza kutoka njeya Nchi” alisema Mhe. Bashungwa aidha Mhe. Bashungwa alitoa rai kwa wananchi na wadau wa sekta yaViwanda na Biashara kuendelea kuunga mkono kwa kununua bidhaa zandani zinazo tengenezwa na wawekezaji wazawa na wazalendo.“Niwaombe watanzania kuendelea kuipa kipaumbele neno ‘MADE INTANZANIA’ utajisikiaje umeenda Nchi za watu ukakuta chombounachotumia kimewekwa nembo ya Tanzania, hakika ni fahari sana”alisema Mhe. BashungwaNaye Mkurugunzi Mkuu wa kiwanda cha Tropical, Ndugu Charles Mlawaameipongeza Serikali ya Tanzania kwa kuendelea kuwaunga mkono nakuwajali katika kuhakikisha sera na lengo la kufikia uchumi wa kati
Nchini ifikapo 2025, kwani mpaka sasa kiwanda hicho kinapata umemewa uhakika kutoka Tanesco.“Nampongeza sana Rais Magufuli kwa kuendelea kutuunga mkono sisiwawekezaji wa ndani, kwetu sisi ni fahari na tutaendelea kuiungamkono Serikali yetu” alisema Bwan. MlawaWaziri Bashungwa katika ziara yake, pia alitembelea kiwanda chaAFRICAB kilichopo Kurasini Jijini Dar es Salaam kinacho jihusisha nautenegezaji wa vifaa vya umeme vya majumbani, kinachomilikiwa naWageni kutoka India.


from MICHUZI BLOG https://ift.tt/2SIZEQW
via
logoblog

Thanks for reading BASHUNGWA: TUUNGE MKONO BIDHAA ZA NDANI ‘MADE IN TANZANIA’

Previous
« Prev Post