Baadhi ya wakenya kunywa maziwa, soda na vitafunio mazishi ya Moi?

  Masama Blog      
Serikali ya Kenya itatoa viburudisho kwa watu 30,000 wa kwanza kufika katika mazishi ya rais wa zamani wa Kenya Daniel arap Moi siku ya Jumatano.

Mratibu wa jimbo la Rift Valley Regional George Natembeya amesema kuwa kutakuwa na viti, soda, maziwa na mikate pamoja na maji kwa watu 30,000 wa kwanza kufika kwenye mazishi na pia watakalishwa kwenye hema.

Bwana Natembeya amesema kuwa waombolezaji waliosalia watakaribishwa tu ndani ya eneo la makazi, lakini hawatapata mahala pa kukaa.

Amesema pia kwamba vitafunio kwa wale watakaohudhuria mazishi wa kwanza vitatolewa: "atakayefika kwanza ndiye atakayepewa wa kwanza ", amesema Bwana Matembeya huku akiwataka waombolezaji kufika mapema kilioni

Usafiri utatolewa kuanzia mji wa Nakuru hadi katika makazi ya Moi ya Kabarak yapata kilomota 20 (sawa na maili 12.4) kutoka Nakuru mjini.

Baadhi ya wakenya kwenye mitandao ya kijamii wamekosoa vigezo kauli hiyo ya serikali ya kutolewa kwa viburudisho vya bure kwa waombolezaji.
 from MICHUZI BLOG https://ift.tt/38iTNXM
via
logoblog

Thanks for reading Baadhi ya wakenya kunywa maziwa, soda na vitafunio mazishi ya Moi?

Previous
« Prev Post