ASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI KWA KUDAIWA KUCHOMA MOTO KITABU CHA QURAAN MKOANI TANGA

  Masama Blog      
NA MWANDISHI WETU,TANGA.

JESHI la Polisi Mkoa wa Tanga linamshikilia mkazi wa Mtaa wa Amboni Kata ya Mzizima Jijini Tanga kwa kuchoma moto kitabu cha Kiislamu cha Juzuu.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga Mrakibu Mwandamizi wa Jeshi la  Polisi Emanuel Minja alithibitisha kukamatwa na mkazi huyo huku akieleza kwamba tukio hilo lilitokea February 8 mwaka huu saa mbili usiku.

Alisema kwamba wao walipata taarifa kwamba huku kwenye mtaa wa Amboni Kata ya Mzizima kuna mtu alichoma Kitabu cha Kiislamu kiitwacho Juzuu na polisi walifika eneo la tukio kwa ufuatiliaji na kumkamata mtuhumiwa huyo

Alimtaja aliyekamatwa na Jeshi hilo kwa kuchoma moto kitabu hicho kitakatifu cha Juzuu ni Emanuel Kuyanga (49) kabila Muha Mkristo na mkulima mkazi wa mtaa wa Amboni.

Akielezea namna tukio hilo lilivyokuwa Kaimu Kamanda huyo alisema kwamba nyumbani kwa Emanuel waifika Athumani Rajabu (14) Mwanafunzi akiwa na wenzake kwa lengo la kuomba mchango wa maulidi baada ya kufika kwa mtu huyo hakuwahamini watoto.

Alisema kwamba watoto hao walilazimika kujieleza huku wakimuonyesha kitabu hicho kitakatifu cha Juzuu hata hivyo Emanuel hakuwaamini watoto hao na kitabu hicho na baada ya kuona hivyo watoto hao walimueleza kwamba kitabu hicho ni kitakatifu na mtu akikichezea anaweza kuwa kichaa au kuota mkia.

Aidha alisema baada ya Emanuel kusikia maneno hayo aliagiza kiberiti kutoka ndani kwake na kupokonya kitabu hiho kisha kuchoma moto ili aone matokeo namna itakayokuwa.

“Hivyo Jeshi la Polisi kwa sasa linamshikilia Emanuel kwa mahojiano na hatua za kisheria zaidi lakini pia nitoe wito kwa wananchi na wageni kwamba Tanga ni shwari na hakuna migogoro ya kidini”Alisema Kaimu Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa Tanga
Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga Mrakibu Mwandamizi wa Jeshi la  Polisi Emanuel Minja
from MICHUZI BLOG https://ift.tt/38fnY2b
via
logoblog

Thanks for reading ASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI KWA KUDAIWA KUCHOMA MOTO KITABU CHA QURAAN MKOANI TANGA

Previous
« Prev Post