AFRICAN LEADING WOMEN IMPACT WAJIPANGA KULETA MABADILIKO 2020

  Masama Blog      
Na Khadija seif, Michuzi Tv
TAASISI inayolenga kumkwamua mwanawake wa kiafrika katika kuleta mabadiliko (African Leading Women Impact’ ) wakishirikiana na wasanii katika tasnia mbalimbali wameungana kwa pamoja na kuhamasisha wanawake wa kitanzania kuleta mabadiliko.

Akizungumza na waandishi wa habari Mkurungezi wa taasisi hiyo Charity Dadi amesema kuwa ukielimisha mwanamke umeelimisha jamii nzima kwa sababu mwanamke ni nguzo ya familia.

“Ni zamu yetu 2020 mwanamke wa kiafrika mwenye ushawishi na muongozo wa matokeo chanya kujifunga mkanda kwenye kuleta mabadiliko ndani ya nchini,” 

Hata hivyo ameeleza kuwa wanalengo la kutembea kila mkoa wakishirikiana na wasanii hao ili kuwajengea uwezo wanawake pamoja na kuwahamasisha na kufanya uthubutu ili waweze kushiriki katika ujasiriamali pamoja na kujitokeza kugombea nafasi mbalimbali za uongozi. 

"Lengo letu kuwatumia wasanii ni kutokana na kuwa vioo vya jamii hivyo ni rahisi kufikisha ujumbe kwa hadhira iliyokusudiwa hasa wanawake wa Kitanzania.

Mmoja wa kamati hiyo ya uhamasishaji  ambae pia ni msanii wa Muziki wa hip hop maarufu Kama witness kibonge amesema mbali na shughuli za kimuziki yeye ni mjasiriamali ambapo ana miradi mingi ambayo anafanya.

"Wanawake tusikate tamaa katika sekta yoyote ile unaweza ukaanzisha miradi mingi kwa wakati mmoja Cha msingi nikuweka malengo na nia kwa kile unachokifanya ili kusukuma gurudumu la uchumi,"

Pia miongoni mwa wasanii watakaoshiriki katika kampeni hiyo ya kumkwamua mwanamke wa kiafrika ni pamoja na Johari, Halima Yahya, Marry Mtemi, Husna Sajent, Vivian Labosh, Maya Mrisho, Tabu Mtingita na wengine wengi.
Mkurugenzi wa taasisi inayolenga kumkwamua mwanamke wa kiafrika ( African Leading Women Impact’ ) Charity Dadi akizungumza na waandishi wahabari pamoja na wasanii wakike wa Muziki pamoja na filamu kuhusiana na kuhamasisha Maendeleo kwa wanawake wa kiafrika.
Attachments area


from MICHUZI BLOG https://ift.tt/2v7togS
via
logoblog

Thanks for reading AFRICAN LEADING WOMEN IMPACT WAJIPANGA KULETA MABADILIKO 2020

Previous
« Prev Post