Ticker

10/recent/ticker-posts

ZOEZI LA UPIMAJI WA DAMU KWA AJILI YA KUTAMBUA WALIOPATA MALARIA KATIKA SHEHIA YA KIKWAJUNI MAJUMBA YA MJARUMANI ZANZIBAR WAFANYIKA


 Daktari Hamadi Khamis Makame akimtoa damu Mtoto Huda Abdalla Abdillahi mkaazi wa Kikwajuni katika Zoezi la utoaji wa Damu kwa ajili ya kupima Malaria yaliogundulika zaidi katika Shehia hio ambapo kiasi cha watu 50 wamegundulika Kikwajuni Majumba ya Mjarumani Zanzibar.
Daktari Hamadi Khamis Makame akimtoa damu Mtoto Omari Mjaka Idarous mkaazi wa Kikwajuni katika Zoezi la utoaji wa Damu kwa ajili ya kupima Malaria yaliogundulika zaidi katika Shehia hio ambapo kiasi cha watu 50 wamegundulika Kikwajuni Majumba ya Mjarumani Zanzibar.
Wananchi mbalimbali waliohudhuria katika  Zoezi la utoaji wa Damu kwa ajili ya kupima Malaria yaliogundulika zaidi katika Shehia hio ambapo kiasi cha watu 50 wamegundulika Kikwajuni Majumba ya Mjarumani Zanzibar.
Meneja Mratibu wa Malaria Unguja na Pemba Abdalla Suleiman akiwa pamoja na Naibu Meneja Faiza Abbas wakishajiisha watu kwenda kutoa Damu  kwa ajili ya kupima Malaria yaliogundulika zaidi katika Shehia hio ambapo kiasi cha watu 50 wamegundulika Kikwajuni Majumba ya Mjarumani Zanzibar.
……………….

Na Khadija Khamis ,Maelezo Zanzibar 

Meneja Mratibu wa Malaria Zanzibar Abdalla Sleiman Ali ameitaka jamii kuweka tahadhari kutokana na ongezeka  la wagonjwa wengi ambao wamegundulika na  vimalea vya  malaria nchini.

Akizungumza katika zoezi la upimaji wa malaria katika kaya mbali mbali za Shehiya ya Kikwajuni Juu amesema takwimu zinaonyesha kuwa kuanzia mwezi wa oktobar, novembar na disemba, jumla ya wagonjwa 33 wamelazwa katika hospitali  kuu ya Mnazimmoja na wagonjwa 4 wamefariki dunia.

Amesema kuwa maeneo yamegundulika uwepo wa watu wenye  ugonjwa huo katika miezi minne waliweza kuwatibu wagonjwa 50 kutoka kikwajuni bondeni wagonjwa 17  kikwajuni juu wagonjwa wengine katika  shehiya mbali mbali  ikiwemo Miembeni,  Kwahani, kwaboko ,wilaya ya kati kaskazini A na B maeneo yote hayo yamegunduliwa kuna wagonjwa wa malaria .

aidha amewasisitiza wananchi kutumia ipasavyo vyandarua pamoja na kusafisha mazingira yaliyowazunguka ili kuepusha mbu kuzaliana na kusababisha  kuzidi kuongezeka kwa ugonjwa huyo nchini.

Alifahamisha zoezi la upimaji damu wa wananchi kutasaidia kugundua mapema wananchi ambao wanamaambukizo ya  malaria na kupatiwa matibabu kwa haraka jambo ambalo litasaidia kuenea kwa maambukizo ya maradhi hayo.

Akieleza sababu za kuenea kwa haraka maradhi hayo alisema kuwa hii inachangia kutokana na utumiaji mdogo wa vyandarua katika jamii .watu kutoka nje ya Zanzibar pia husababisha kuigiza maradhi hayo pamoja mabadiliko ya hali ya hewa joto na mvua husababisha unyevu unyevu na kutuwama maji  kuwa  mazalio ya mbu .

Hata hivyo alifahamisha baadhi ya wavuvi waliopimwa ambao wanaotokea katika maeneo hayo kati ya wavuvi 29,waliopimwa 19 wamegundulika na vimalea hivyo  .

Akitoa wito kwa jamii mtu akijigundua na ishara na  dalili afike haraka katika vituo vya afya kwa kupatiwa matibabu asikae nyumbani ,kukaa nyumbani kutahatarisha maisha yake.

Nae Daktari kutoka Timu ya Malaria kwa Wilaya ya Mjini  Hamad Khamis Ali amesema tokea kuanza kwa  zoezi hilo jumla ya watu watano wameshagundulika kuwa na vimelea vya ugonjwa wa malaria.

zoezi hilo litafanyika kwa siku mbili kwa kila haya katika maene ya kikwajuni juu na kikwajuni bondeni kutokana na kuzuka kwa wagonjwa wengi katika eneo hilo pamoja na kuonekana kumekuwa na  mazingira hatarishi.


from MICHUZI BLOG https://ift.tt/35lzwyN
via

Post a Comment

0 Comments