ZIMEBAKI SIKU TATU, WATU ZAIDI YA ELFU SITA HAWAJATUMIA NAMBA ZA UTAMBULISHO KUSAJILI LAINI ZA SIMU KWA ALAMA ZA VIDOLE

  Masama Blog      
Na Avila Kakingo, Globu ya Jamii
IKIWA zimebaki siku tatu za kufungwa simu zisizosajiliwa kwa alama za vidole kumbe kuna namba za utambulisho wa Taifa 6,806,096 hazijatumika kusajili laini za simu kwa alama za vidole mpaka sasa.

Hayo ni kufuatia taarifa iliyotolewa na Kitengo cha Mawasiliano na Hifadhi Hati, Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) jijini Dodoma Jana.

Taarifa hiyo inaeleza kuwa Utambuzi wa Watu, uzalishaji wa Namba za Utambulisho wa Taifa na vitambulisho, na ugawaji wake, kwa wananchi zinazotumika kusajili laini za simu kwa alama za vidole na huduma nyingine zinazohitaji utambulisho. 

Imesema kuwa hadi Januari 15, 2020, Mamlka ya Vitambulisho vya Taifa imezalisha idadi kubwa ya namba zautambulisho wa Taifa.

Hivyo, Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) inatoa rai kwa watu wote ambao wamekwishapata namba za utambulisho wa Taifa wakasajili laini zao za simu ili wasifungiwe laini zao ifikapo Januari 20, 2020, kama Serikali ilivyoelekeza kwa sababu, namba ya utambulisho wa Taifa, inatosha kusajili laini hata kama mwombaji hajapata Kitambulisho cha Taifa.

Taarifa hiyo inaeleza kuwa Katika kurahisisha kuwapatia namba za utambulisho wa Taifa wananchi, NIDA imebuni njia mbalimbali ambazo ni kupeleka namba za utambulisho wa Taifa katika ngazi ya Kata na Vijiji, kutumia USSD *152*00#, kutuma ujumbe mfupi wa simu kwenda namba 15096, ambapo mwombaji anatakiwa kuandika jina la kwanza*jina la mwisho*tarehe, mwezi, mwaka wa kuzaliwa* jina la kwanza la mama*jina la mwisho la mama na huduma hii ni bure. 

Aidha, wananchi pia wanaweza kupata namba za utambulisho wa Taifa katika ofisi za NIDA zilizopo karibu yao au vituo vya muda vya Mamlaka.

Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa inapenda kuwajulisha Wageni Wakaazi wanaoishi nchini kwa zaidi ya miezi sita nao wajitokeze kusajiliwa ili wapate namba za utambulisho wa Taifa na kusajili laini zao kwa alama za vidole. 

Kwa Upande wa Wageni wanaoishi nchini chini ya miezi sita wanatakiwa kusajili laini zao kwa kutumia Pasi za Kusafiria za Nchi zao na kufuata utaratibu uliowekwa na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA).


from MICHUZI BLOG https://ift.tt/387HQUy
via
logoblog

Thanks for reading ZIMEBAKI SIKU TATU, WATU ZAIDI YA ELFU SITA HAWAJATUMIA NAMBA ZA UTAMBULISHO KUSAJILI LAINI ZA SIMU KWA ALAMA ZA VIDOLE

Previous
« Prev Post