ZAIDI YA WANAFUNZI 30 WACHAGULIWA SHULE ZA VIPAJI MAALUM TANDAHIMBA.

  Masama Blog      

Mkuu wa Wilaya ya Tandahimba Sebastian Waryuba amewataka  wanafunzi ambao wamechaguliwa kidato cha kwanza katika shule maalum wakaendeleze vipaji vyao kwa kuweka jitihada katika masomo.

Amesema kuwa kuchaguliwa katika shule za vipaji  hakuwafanyi washindwe kuongeza jitihada ili waweze kufika mbali zaidi.

Hayo ameyasema katika hafla yake maalum kwa ajili ya kuwapongeza wanafunzi waliochaguliwa kwenda shule za vipaji maalum ndani ya Wilaya yake

"Msizembee mkajitahidi Kusoma  ili mfikie malengo ,kwa ninyi watoto wakike msikubali mtu awakatishe masomo yenu lazima mfikie malengo yenu ya kufika mbali,"alisema Waryuba

Hata hivyo aliwapongeza wazazi na walimu kwa kushirikiana vizuri na kuwafikisha wanafunzi  katika hatua ya kuigwa

"Katika hafla hii nimefarijika kuungana nanyi walimu,wazazi na wanafunzi ili kuwatia moyo watoto wetu ambao wamefanya vzr na kuwapa zawadi"alisema Waryuba

Katika halmashauri ya Tandahimba zaidi ya wanafunzi 30 wamechaguliwa kwenda shule za vipaji maalum.

Mkuu wa Wilaya ya Tandahimba Sebastian Waryuba akisistiza Jambo
Mkuu wa Wilaya ya Tandahimba Sebastian Waryuba  akimpongeza mmoja wa Wanafunzi ambao wamechaguliwa kidato Cha kwanza katika shule maalum wakaendeleze vipaji vyao kwa kuweka jitihada katika masomo.
 Wageni waalikwa


from MICHUZI BLOG https://ift.tt/2ZHIR2H
via
logoblog

Thanks for reading ZAIDI YA WANAFUNZI 30 WACHAGULIWA SHULE ZA VIPAJI MAALUM TANDAHIMBA.

Previous
« Prev Post