YANGA YAITUPIA 'MZIGO' WA LAWAMA BODI YA LIGI

  Masama Blog      
Na Yassir Simb,Michuzi Globu.

Uongozi wa Klabu ya Yanga imeitupia lawama bodi ya ligi (TPLB) kwa kubadilisha tena sehemu ya mchezo wao dhidi ya Wakulima wa Alizeti Singida United kutoka dimba la Sheikh Amri Abeid jijini Arusha na kuurejesha mpambano huo katika dimba la Namfua mkoani Singida, ikiwa ni muda mfupi tu baada ya wao wakiwa tayari wamefanya maandalizi ya awali.

Katibu Mkuu wa Yanga, Dk. David Luhago amesema tayari wamefanya maandalizi ya 'booking' ya usafiri wa ndege na kulipa sehemu ya pesa (advance) katika hoteli watakayo fikia, hivyo hawaelewi ni namna gani watarudisha gharama zao kufuatia mabadiliko hayo.

Dk. Luhago amesema kwa kawaida ikiwa kuna mabadiliko ya ratiba ya mchezo, taarifa inapaswa kutolewa saa 48 kabla lakin bodi ya Ligi haikufanya hivyo na kuwashtukiza kuwaambia mchezo huo utapigwa mkoani Singida nasi jijini Arusha tena. 

"Bodi ya ligi ilituandikia barua kuwa mchezo wetu dhidi  dhidi ya Singida United utapigwa uwanja wa Sheikh Amri Abeid Arusha lakini wamebadili tena, kuwa tutaenda Singida katika uwanja wa Namfua wakati sisi tushalipa gharama za awali,taarifa ilipaswa kutolewa mapema , sisi tumejiandaa kuwa tunasafiri kwenda Arusha." alisema Dk Luhago.


from MICHUZI BLOG https://ift.tt/30wZpLa
via
logoblog

Thanks for reading YANGA YAITUPIA 'MZIGO' WA LAWAMA BODI YA LIGI

Previous
« Prev Post