WILAYA ZAIDI YA 20 ZAKABILIWA NA TATIZO LA UDUMAVU KWA WATOTO NA AKINA MAMA WAJAWAZITO

  Masama Blog      
Wilaya ya Lwangwa Mkoani Lindi imetajwa kuwa na asilimia saba ya lishe duni ikifutaiwa na Wilaya ya Tandahimba Mkoani hapo yenye asilimia 6.5.

Uchunguzi uliofanywa na na taasisi inayojihusisha na utoaji wa elimu kwa wanawake, vijna na watoto kuhusu masuala ya lishe, udumavu pamoja na fistula (Fureo) umeonyesha kuwa Wilaya zaidi ya 20 zinakabiliwa na tatizo la udumavu kwa watoto na akina mama wajawazito kutopata lishe inayostahili .

Wilaya hizo ni Mbarali, Rungwe, Kibiti, Rufiji, Bagamoyo, Chalinze, Ilala, Ubungo, Kilolo, Mufindi, Lwangwa, Nachingwea, Tandahimba, Wanging’ombe, njombea, Ifakara, Kilolo, Magu, Njombe, Chato, Geita, Shinyanga manispaa na Kahama.

Raia hiyo imetolewa na Mjumbe wa tasisi hiyo Kelvin Haule jijini Dodoma wakati akiongea na waandishi wa habari amesema kuwa wilaya hizo hali ya lishe ni asilimia 24 pekee huku wilaya ya Lwangwa ikiwa na asilimia 7 ya udumavu.

Bw.Haule amesema kuwa katika uchunguzi huo walibaini kuwa watoto wenye umri wa kati ya miezi sita hadi 23 wanakabiliwa na changamoto ya upataaji wa lishe bora kutokana na kukosenaka kwa elimu ya kutosha matumizi ya bora ya vyakula.

“Hali ya lishe katika wilaya hiyo si ya kuridhisha kwani zipo kwenye asilimia 24 tu, na kati ya hizo Wilaya abayo ina tatizo hili kwa kiwango kikubwa ni Wilaya ya Lwangwa yenye asilimia 7 ikifutaiwa na Tandahimba asilimia 6.8,”amesema Bw.Haule

“Ili kukabiliana na changamoto hiyo ambayo wakati mwingine inasababisha  vifo ni lazima wadau mbalimbali wa afya wawekeza kwenye utoaji wa elimu jamii na si kuiachia serikali pekee,”.

Aidha amesema kuwa  katika kuunga mkoni Juhudu za serikali za utoaji wa elimu kuhusu masuala ya afya wameamua kuanzisha mradi ambao watakutekeleza kwa muda wa miezi nane katika Wilaya hizo.

Hata hivyo amesema kuwa kila wilaya  wanatarajia kuwafikia wananchi 120 wakiamini elimu hiyo itawafikiwa watu wengi zaidi baada ya mradi huo kukamilika.

Bw.Haule amesema kuwa  mradi huo unalenga kuongeza kiwango cha upatikanaji wa lishe kutoka asilimia 24 hadi kufikia asilimia 50 na utatekelezwa kwa gharama ya zaidi ya Sh258.8 milioni.

Naye Mkurugenzi wa taasisi hiyo Davidi Msuya amesema  kuwa msingi mkubwa wa mradi huu ni kuhakikisha wanakomesha tatizo la fistula kwa wanawake na utapiamlo kwa watoto.

Msuya amesema kuwa mradi huo wanatarajia kuuza Januari 28,2020 ukiusisha wataalamu mbalimbali wa masuala ya afya.
 Mkurugenzi wa taasisi hiyo Davidi Msuya,akisisitiza jambo kwa waandishi wa habari kuhusiana na uchunguzi wa utafiti walioufanya katika wilaya mbalimbali kuhusu lishe
 Mjumbe wa taasisi inayojihusisha na utoaji wa elimu kwa wanawake, vijna na watoto kuhusu masuala ya lishe, udumavu pamoja na fistula (Fureo) Bw.Kelvin Haule,akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani)


from MICHUZI BLOG https://ift.tt/38qfIMz
via
logoblog

Thanks for reading WILAYA ZAIDI YA 20 ZAKABILIWA NA TATIZO LA UDUMAVU KWA WATOTO NA AKINA MAMA WAJAWAZITO

Previous
« Prev Post