WILAYA YA IKUNGI YATEKELEZA AGIZO LA RAIS KWA KUTENGENEZA MADAWATI 1600

  Masama Blog      

Mkuu wa Wilaya ya Ikungi, Edward Mpogolo (kushoto) akimkabidhi madawati Mwakilishi wa Mwalimu Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Puma, Mwalimu Amani Kipandwa katika hafla iliyofanyika juzi. Wa pili kushoto anayeshuhudia makabidhiano hayo ni Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi, Justice Kijazi na kulia ni Diwani wa Kata ya Ikungi, Abel Nkuhi.

Wanafunzi wakiwa katika hafla hiyo ya kupokea madawati.
Mkurugenzi wa halmashauri hiyo Justice Kijazi  akitoa taarifa fupi wakati wa hafla ya kukabidhi  madawati hayo.
Makabidhiano ya madawati hayo yakiendelea.

Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Ikungi, Orda Phabiani akizungumza.
Wanafunzi wakiwa katika hafla hiyo ya kupokea madawati.


Na Dotto Mwaibale, Singida

HALMASHAURI ya Wilaya ya Ikungi mkoani Singida
imetekeleza agizo la Rais John Magufuli kwa kutengene
za madawati 1600 na kuhakikisha wanafunzi wote
walioanza kidato cha kwanza mwaka huu wanakwenda
shuleni na wanakaa kwenye viti.

Madawati hayo yamepatikana kutoka halmashauri hiyo
na kuungwa mkono na wadau wa maendeleo pamoja na
wabunge Elibariki Kingu na Miraji Mtaturu.

Mkuu wa Wilaya ya Ikungi, Edward Mpogolo
akizungumza wakati akigawa madawati hayo
alimpongeza Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo,
Justice Kijazi na watendaji wake kwa kazi hiyo kubwa
walioifanya ya kutengeneza madawati hayo.

“Kwa nchi nzima halmashauri yetu imekuwa ya 78 kati
halmashauri 195 zilizopo ni jambo la kujivunia na naamini
kabisa ipo siku na sisi tutashika
nafasi ya kwanza” alisema Mpogolo.

Mpogolo alisema wanafunzi wote 4, 517 waliochaguliwa
kuanza kidato cha kwanza watakwenda shuleni na
watakaa kwenye viti.

Alisema wadau wa maendeleo waliochangia ununuzi
wa madawati hayo hawakufikiria familia zao bali
waliwafikiria wanafunzi hao kwani lengo la halmashauri
hiyo ni kuhakikisha madawati yote 3900 yanapatikana
na kuwa watoto hao wote wanafika chuo kikuu.

Mpogolo alitumia nafasi hiyo kumshukuru Rais Magufuli
kwa kuipa wilaya hiyo sh.1.3 Bilioni kwa ajili ya
kugharamia elimu pasipo malipo na sh.400 milioni
za kugharamia ujenzi wa miundo mbinu.

Mkurugenzi wa halmashauri hiyo Justice Kijazi
akitoa taarifa fupi wakati wa hafla ya kukabidhi
madawati hayo alisema fedha za kununua madawati
hayo zilitoka katika mapato ya ndani na kuchangiwa
na wadau wa maendeleo ambapo Benki ya NMB ilitoa
viti 100 na meza, Shirika la Hifadhi ya Taifa (TANAPA)
sh. milioni 24 pamoja na wabunge wa Jimbo la Singida
Mashariki na Magharibi ambao kila mmoja alitoa
sh. milioni tano.

Alisema hatua hiyo waliifikia kufuatia ongezeko
kubwa la ufaulu wa watoto na kuhakikisha wote wanakwenda shuleni na kuwa na viti vya kukalia.


from MICHUZI BLOG https://ift.tt/2R5oTft
via
logoblog

Thanks for reading WILAYA YA IKUNGI YATEKELEZA AGIZO LA RAIS KWA KUTENGENEZA MADAWATI 1600

Previous
« Prev Post