WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA AWATAKA VIONGOZI WA SERIKALI KUWATUMIKIA WANANCHI BILA UBAGUZI

  Masama Blog      
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, akiweka jiwe la msingi la Huduma za Mama na Mtoto, Bambi mkoani Kusini Unguja. Januari 17, 2020. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, akiangalia kitanda cha wazazi, baada ya kuweka jiwe la msingi la Huduma za Mama na Mtoto, Bambi mkoani Kusini Unguja. Januari 17, 2020. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, akiwahutubia wananchi, baada ya kuweka jiwe la msingi la Huduma za Mama na Mtoto, Bambi mkoani Kusini Unguja. Januari 17, 2020. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).

Na Maryam Kidiko .

Waziri mkuu wa Jamuhuri ya muungano wa Tanzania Mhe, Kassim Majaliwa amewataka Viongozi wa Serikali kuwatumikia wananchi bila ya ubaguzi na kuhakikisha wanapata huduma muhimu za kijamii ili kutatua changamoto zinazowakabili.

Hayo ameyasema alipokuwa akizungumza na Viongozi mbali mbali wakati akifanya ziara za kuangalia miradi ya maendeleo ikiwemo kuzindua Jengo la huduma za Mama na Mtoto Bambi . .

Amesema kila mtumishi wa umma ahakikishe anafanya kazi kwa vitendo na kuwajibika kutokana na majukumu waliopangiwa ili kuhakikisha wananchi wanapata haki zao za msingi.

Waziri Kassim ameitaka Serikali ya mkoa wa kusini Unguja kuweka mpango mkakati wa kuwafatilia wananchi wao katika vijiji vyao ili kujua changamoto zinazowakabili na kuzitatua kwa haraka.

Amesema kuwa Viongozi lazima waweke mpango mkakati wa kukuza uchumi na huduma za kijamii zikiwemo skuli ,vituo vya afya ,kilimo na kukuza utalii nchini ili taifa liweze kuingiza fedha za kigeni zitakazowasaidia wananchi katika huduma muhimu.

Hata hivyo amesema katika swala la usalama Serikali ihakikishe inaweka usalama wa kutosha wa kulinda raiya na nchi kwa jumla ili kuwepo na amani na utulivu.

Akitoa Taatifa fupi ya Mkoa Mkuu wa Mkoa wa kusini Unguja Ayoub Mohamed Mahmuod amesema kwa upande wa mkoa huo umejipanga kuhakikisha unatatua na kushughulikia changamoto zote walizokuwa nazo wananchi .

Ziara hiyo ya siku moja imetembelea miradi mitano ya kimaendeleo ikiwemo kuzindua kituo cha afya ya kijiji kizimkazi Dimbani , ukaguzi wa maabara ya sayansi Bwejuu,kukagua kilimo cha kisasa jozani na kuzindua huduma ya mama na mtoto Bambi.


from MICHUZI BLOG https://ift.tt/2tl9ajy
via
logoblog

Thanks for reading WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA AWATAKA VIONGOZI WA SERIKALI KUWATUMIKIA WANANCHI BILA UBAGUZI

Previous
« Prev Post