Ticker

10/recent/ticker-posts

WAZIRI BITEKO AKIFUNGA KIWANDA BUBU CHA UCHENJUAJI DHAHABU

Baaadhi ya mifuko iliyojazwa kemikali za kuchenjulia dhahabu. (kaboni)


Waziri wa Madini Doto Biteko kushoto akichungulia chumba kilichosimikwa mtambo wa kuchenjulia madini ya dhahabu, kulia ni mwenyekiti wa Kijiji cha Bunanga January Luhamba.


Waziri wa Madini Doto Biteko kulia akiwa amebeba furushi la kemikali za kuchenjulia madini ya dhahabu (kaboni) kushoto ni Afisa Mtendaji wa Kijiji cha Bunanga Kajanja Kajanja.
Waziri wa Madini Doto Biteko kulia akimuelekeza mwenyekiti wa Kijiji cha Bunanga January Luhamba sehemu ya kusaini.

Waziri wa Madini Doto Biteko kushoto akimuelekeza jambo
Mkuu wa jeshi la Polisi wa kituo cha Bugarama

Maafisa wa Madini wa Wilaya ya Kahama wakiweka sildi katika mlango wa kiwanda bubu cha kuchenjulia madini ya dhahabu.
*******************************

Na Tito Mselem, Kahama

Waziri wa Madini Doto Biteko amekifunga kiwanda bubu cha kuchenjua madini ya dhahabu kilichofunguliwa kinyemela katika Kijiji cha Bunanga kata ya Bugarama Halmashauri ya Msalala Wilayani Kahama. 

Kiwanda hicho kinachomilikiwa na Simoni Shule kipo katikati ya makazi ya watu ambapo kinahatarisha maisha ya watu na kuharibu mazingira baada ya kutiririsha kemikali za sumu kwenye makazi ya watu.

Waziri Biteko alisema, licha ya serikali kuboresha Sekta ya Madini kwa wachimbaji na wafanyabiashara wadogo wa madini nchini, imebainika kuwa wapo ambao wamekuwa wakifanya shughuli za uchenjuaji wa madini ya dhahabu ikiwemo kuanzisha viwanda bubu kinyume na taratibu na kuikosesha serikali mapato.

Hayo yalibainishwa Januari Mosi mwaka 2020 na Waziri Biteko baada ya kufanya ziara ya kushtukiza katika kijiji cha Bunanga kata ya Bugarama Halmashauri ya Msalala Wilayani Kahama na kubaini kiwanda bubu cha kuchenjua madini ya dhahabu kilichopo katikati ya makazi ya watu.

“Kiwanda hiki kipo hapa katika nyumba hii kwa kipindi cha zaidi ya miezi 7 kikiendelea kufanya kazi bila kufuata Sheria na Taratibu zilizopo na kuipotezea Serikali mapato mengi, hivyo tutachukua hatua kali za kisheria kwa mmiliki wa mtambo huu ili iwe fundisho kwa wengine wenye tabia chafu kama hii,” alisema Biteko.

Aidha, Waziri Biteko aliwataka viongozi wa vijiji na mitaa wilayani humo kuhakikisha wanawafichua wafanyabiashara wanaojihusisha na biashara haramu ya madini ambazo zinafanyika katika makazi ya watu kinyume na Sheria na kuikosesha Serikali mapato.

“Niwaagize viongozi wote wa ngazi zote Nchi nzima kuhakikisha mnasimamia na kuthibiti vitendo vya biashara haramu ya madini ambavyo vinaendelea kufanywa na baadhi ya watu wasio waaminifu katika maeneo mbalimbali nchini, alisema Waziri Biteko.

Wakati huo huo, Waziri Biteko aliliagiza jeshi la polisi la Halmashauri ya Msalala kumkamata na kumuhoji Afisa Mtendaji wa kijiji cha Bunanga Kajanja Kajanja na Mke wa mwenye nyumba iliyobainika kuwa na mtambo wa kuchenjulia dhahabu unaomilikiwa na Simoni Shule
kuhusiana na kuhusishwa na tukio hilo.

Katika ziara hiyo mifuko zaidi ya 44 ya kemikali zinazotumika kuchenjulia madini ya dhahabu (Kaboni) imekamatwa katika kiwanda hicho inayodhaniwa kuwa na madini ya dhahabu, huku mashine hiyo yenye uwezo wa kubeba kilo 500 za Kaboni ikiwa tayari imewekewa
mzigo kwaajili ya kuanza kazi.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Kijiji cha Bunanga Januari Luhamba, alisema, baada ya kugundua shughuli zinazofanywa na kiwanda hicho katikati ya makazi ya watu, alitoa taarifa kwa mamlaka za kisheria ikiwemo polisi kuhusiana na uwepo wa kiwanda hicho katika eneo lake lakini hakuona hatua yoyote iliyochukuliwa kwa wahusika.

“Kiwanda hiki kipo katika nyumba hii kwa muda mrefu sasa, kuna vijana wageni wengi wamekuja kufanya kazi ya kuchenjua dhahabu katika kiwanda hiki, viongozi wote wa eneo hili wanajua tumelalamika sana kuhusiana na kumwagwa ovyo kwa maji yenye kemikali kwenye makazi
yetu,” alisema.Luhambo.


from MICHUZI BLOG https://ift.tt/36m4Sqc
via

Post a Comment

0 Comments