Ticker

10/recent/ticker-posts

Wavamizi wa Kiwanja cha Programu ya Urithi na Ukombozi Bara la Afrika Mwabwepande watakiwa Kuondoka Haraka

Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Habari,Utamaduni Sanaa na MIchezo Dkt.Ally Possi (alievaa kofia) leo akikagua eneo la Kiwanja ambapo kutajengwa Kituo cha Kikuu cha Kimataifa cha Programu ya Urithi wa Ukombozi wa Bara la Afrika lenye ukubwa wa ekari 65 lililopo katika Mtaa wa Mji Mpyaa Mwabwepande jijini Dar es Salaam,watatu kushoto ni Kaimu Mkurugenzi Idara ya Maendeleo ya Sanaa katika Wizara ya Habari, Utamaduni ,Sanaa na Michezo Bibi.Joyce Fisoo na wa kwanza kulia
ni Kaimu Mkurugenzi Msaidizi Sehemu ya Urithi na Maadili ya Taifa kutoka Wizara ya Habari, Utamaduni ,Sanaa na Michezo Bw.Boniface Kadili.
Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Habari,Utamaduni Sanaa na MIchezo Dkt.Ally Possi (aliyevaa kofia)wa akikikagua baadhi ya barua za mmoja wa watu wanapoishi alizoziandika Wilaya ya Kinondoni akidai eneo hilo kuwa ni la wazazi wake, alipofanya ziara ya kukagua kiwanja hicho leo jijini Dar es Salaam, Kiwanja hicho kitakacho jengwa, Kituo Kikuu cha Programu ya Urithi wa Ukombozi wa Bara la Afrika ambapo alikuta kuna wananchi wamevamia wanaishi katika eneo hilo mbali na kuwa Wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo kuwa wameshapewa hati yakiwanja hicho.
Baadhi ya muonekano wa nyumba za wavamizi wanaoishi katika eneo la la Kiwanja cha kujengwa Kituo Kikuu cha Programu ya Urithi wa Ukombozi wa Bara la Afrika kilichopo katika eneo la Mabwepande jijini Dar es Salaam alizozikuta Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Habari,Utamaduni Sanaa na MIchezo Dkt.Ally Possi (hayupo pichani) alipofanya ziara yake leo katika eneo hilo kufuatilia kiwanja hicho ambacho wizara yake inampango wa kuweka uzio.


from MICHUZI BLOG https://ift.tt/39GjLWs
via

Post a Comment

0 Comments