WATAALAM WA KILIMO CHA UMWAGILIAJI WAJADILI MIRADI YA UMWAGILIAJI INAVYOWEZA KUWA ENDELEVU.

  Masama Blog      
Na Ripota Wetu, DODOMA

Wataalam wa kilimo cha umwagiliaji wameendelea na majadiliano Jijini Dodoma huku, wakibadilishana mawazo na uzoefu kuhusiana na Mradi wa kuwajengea uwezo wakulima na wataalam katika Kilimo cha Umwagiliaji wakijikita zaidi katika shughuli za mradi huo,mafanikio na Changamoto na namna ya kutatua changamoto hizo ambazo zinaweza kupelekea Mradi huo kuwa endelevu hata baada ya muda wake kufikia mwisho.

Wataalam hao walifanya mawasilisho ya Mpango kazi kupitilia utekelezaji wa mradi, kama vile kazi za upembuzi yakinifu katika miradi ya kilimo cha umwagiliaji ambayo hufanyika kabla ya mradi kuanza na mradi kutekelezeka, jambo ambalo linapelekea ubora na uimara wa miundombinu ya umwagiliaji.

Sambamba na hilo, mawasilisho pia yalilenga katika majadiliano yaliyohusu tathmini na ufuatiliaji katika swala zima la matumizi na matunzo ya miundombinu ya kilimo cha umwagiliaji hasa katika eneo la matunzo ya miundmbinu hiyo.

Mradi huo ulianza kazi kwa awamu ya kwanza kutoka December 2010 mpaka June 2014, awamu ya pili kutoka August 2015 mpaka August 2019 na kuongezewa muda kuanzia September 2019 mpaka August 2020 ambapo mradi huo unaofadhiliwa na Shirika na Kimataifa la maendeleo la Japan (JICA) kwa kushirikiana na Serikali ya Tanzania utakwisha muda wake. 
 Washiriki katika mkutano wa wadau wa kubadilishana mawazo ya kitaalam kuhusiana na Mradi wa kuwajengea uwezo wataalam na wakulima katika kilimo cha umwagiliaji,wakiwa katika makundi tofauti wakijadili kuhusu mafanikio, changamoto na namna ya kutatua changamoto hizo na namna ambavyo mradi huo unaweza kutekelezwa na kuwa endelevu.
 Katika Picha Wataalam wakisikilza mawasililisho katika mkutano wa wadau wa kubadilishana mawazo ya kitaalam kuhusiana na Mradi wa kuwajengea uwezo wataalam na wakulima katika kilimo cha umwagiliaji, unaendela Jijini Dodoma.
 Picha ikionesha wataalam washiriki katika mkutano wa kubadilishana mawazo kuhusu mradi wa kujengea uwezo wakulima na wataalam katika masuala ya Kilimo cha Umwagiliaji wakijadili maswala ya utekelezaji wa mradi unaokaribia kuisha muda wake.
Bw.  Remigius Rushomesa, Kaimu Mkurugenzi Idara ya Uendeshaji kutoka Tume ya Taifa ya Umwagiliaji, akiongea na waandishi wa habari hawapo pichani, kuhusu namna ambavyo mradi wa kuwajengea uwezo wakulima na wataalam katika kilimo cha  umwagiliaji unavyoweza kuwa endeleevu hata baada ya kuisha muda wake.from MICHUZI BLOG https://ift.tt/37IZYEr
via
logoblog

Thanks for reading WATAALAM WA KILIMO CHA UMWAGILIAJI WAJADILI MIRADI YA UMWAGILIAJI INAVYOWEZA KUWA ENDELEVU.

Previous
« Prev Post