Waogeleaji 35 wa Bluefins kuwania medali Morogoro

  Masama Blog      
 Jumla ya waogeleaji 35 wa timu ya Bluefins watashindana katika mashindano ya kwanza ya kuogelea ya mwaka 2020 yaliyopangwa kufanyika mkoani Morogoro.

Mashindano hayo yanayoshirikisha jumla ya klabu tano, yameandaliwa na shule ya kimataifa ya Morogoro (MIS) na kuidhinishwa na chama cha kuogelea nchini (TSA).

Muasisi na kocha mkuu wa timu ya Bluefins, Rahim Alidina aliwataja waogeleaj wa kike kuwa ni Aliyana Kachra, Zainab Moosajee, Maryam Ipilinga, Alexis Misabo, Aminaz Kachra, Lina Goyayi, Muskan Gaikwad, Filbertha Demello, Niharika Mahapatra, Yumna Hassan na Natalia Ladha.

Kwa upande wa wavulana ni Mohammadhussein Imran, Kaysan Kachra, Sahal Harunani, Moiz Kaderbhai, Jay Govindji,Raihan Abdullatif, Hassan Harunani, Idris Zavery, Isaac Mukani, Kabeer Lakhani, Salman Yasser na Gervas Sayi.

Pia katika orodha ya wavulana ni , Delbert Ipilinga, Zac Okumu, Adam Patwa, Qais Kanji, Kahil Walli, Christian Fernandes, Avinav Mahapatra, Aaron Akwenda, Shuneal Bharwani, Enrico Barretto, Burhanuddin Gulamhussein na Rayyan Khan.

Alisema kuwa katika kuwapa uzoefu, klabu yao imewajumuisha waogeleaji wenye umri mdogo kabisa ambaowatashindana na wenye umri mkubwa.

“Tuna waogeleaji wenye umri wa miaka 11 na chini ambapo watashinada na wenye umri mkubwa, hapa wanatafuta uzoefu mbali ya kusaka medali,” alisema Alidina.

Alisema kuwa staili mbalimbali za kuogelea kama Freestyle, Backstroke, Breaststroke, Butterfly, Individual medley na Medley Relays zitashindaniwa.

“Mwaka jana mwishoni, tulimaliza katika nafasi ya pili katika mashindano ya Taifa ya vijana yaliyoandaliwa na TSA, lengo letu katika mashidanoya Morogoro ni kufanya vyema, waogeleaji wana morali ya hali ya juu ya kuleta mafanikio,” alisema. Mbali ya Bluefins, klabu nyingine ambazo zitashindana katika mashindano hayo ni, Dar Swim Club, Taliss- IST, Champion Rise na wenyeji Mis Piranhas.


from MICHUZI BLOG https://ift.tt/38a0v26
via
logoblog

Thanks for reading Waogeleaji 35 wa Bluefins kuwania medali Morogoro

Previous
« Prev Post